Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Mwili wa kichanga waokotwa jalalani

-
Rehema Mwinyi.

Mwili wa mtoto mchanga wa umri wa miezi miwili umeokotwa ukiwa kwenye dampo la taka pale Mwananyamala Jijini.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mark Kalunguyeye, amesema tukio hilo limejiri majira ya saa 4:00 asubuhi pale Mwananyamala Kwa Msisiri Jijini.

Akasema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema, polisi walifika eneo hilo na kuukuta mwili huo ukiwa umefungwa kwenye taulo na kisha kuviringishwa na khanga juu yake.

Akasema baada ya kuhakikisha hakuna mtu aliyemuona, mwanamke aliyefanya unyama huo aliutupa mwili huo kwenye dampo hilo kabla ya kuingia mitini.

Kamanda Kalunguyeye akasema Polisi wapo katika msako mkali wa kumtafuta mwanamke huyo ili afikishwe katika vyombo vya sheria.

Katika tukio jingine, watu wawili wamekamatwa na polisi baada ya kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya.

Akasema, watu hao walikamatwa majira ya saa 1:00 asubuhi eneo la Stendi ya Mbezi wakiwa na kete nane za madawa ya kulevya.

Akawataja watu hao kuwa ni Evance Jackson. 20, na Rajabu Jumanne, 21.

Akasema, watu hao watafikishwa Mahakamani haraka baada ya kukamilika kazi ya kuwahoji kuhusiana na tukio hilo.

Leave a Reply