Mama mmoja nchini Marekani amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne akidai walikuwa wame wameingilwa namashetani wabaya.
Banita Jacks, 33, wa Washington nchini Marekani amefunguliwa mashtaka manne ya mauaji ya watoto wake wanne wa kike wenye umri kati ya miaka mitano na 17. Banita alikamatwa nyumbani kwake akiishi na mabaki ya miili ya watoto wake ambao maiti zao zilikuwa zikiozea ndani ya nyumba hiyo. Banita alidai kuwa watoto hao walikuwa na mashetani wabaya na walikufa mmoja mmoja wakiwa usingizini. Ndugu wapatao 30 wa familia ya Banita waliohudhuria kesi hiyo mahakamani waliondoka mahakamani kimya kimya bila kutaka kusema chochote. Miili ya watoto hao iligundulika wakati polisi walipoingia nyumbani kwa mama huyo kusini mashariki mwa Washington mwezi januari mwaka jana. Banita aliwaambia wapelelezi kuwa watoto wake walikuwa wakimilikiwa na mashetani wabaya na walianza kufariki mmoja mmoja wakiwa usingizini katika muda wa siku saba. Banita aliwaambia pia wapelelezi hao kuwa aliwanyima chakula watoto wake hao kwa muda mrefu kabla ya vifo vyao. Mchunguzi wa mambo ya kidaktari, Dr. Marie-Lydie Pierre-Louis alisema kuwa kwa kuangalia vielelezo vya idadi kubwa ya wadudu waliokutwa kwenye maiti hizo, miili ya watoto hao ilikuwa ndani ya nyumba aliyokuwa akikaa mama huyo kwa zaidi ya siku 15 kabla ya kugundulika. Polisi walisema kuwa Banita alizuga amehama kwenye nyumba aliyokuwa akikaa kwa kufunga mapazia yote ya nyumba yake na kuacha kulipa bili za umeme na kuacha barua zake zirundikane mbele ya nyumba yake huku yeye akitumia mlango wa nyuma kutokea. Banita huenda akafungwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia. SOURCE:nifahamishe.com | ||