Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Kondoo Azaliwa Akiwa na Sura ya Binadamu

-
Rehema Mwinyi.



Kondoo aliyezaliwa nchini Uturuki akiwa na sura ya binadamu amewashangaza mamia ya watu duniani na kuwa gumzo kwenye vyombo mbali mbali vya habari duniani.
Kondoo huyo aliyezaliwa akiwa amefariki ana sura kama ya binamu lakini mwili wake ni kama wa kondoo.

Kondoo huyo alizaliwa katika zahanati ya mifugo katika kijiji kimoja katika mji wa Izmir nchini Uturuki.

Erhan Elibol, bwana mifugo aliyemzalisha kwa njia ya upasuaji kondoo aliyekuwa na mimba, alielezea mshtuko aliopata baada ya kuona kichanga cha kondoo kilichozaliwa kina sura inayofanana na binadamu.

"Nimewahi kuona maumbile mbali mbali ya ajabu ya ng'ombe na kondoo, nimewahi kuona ng'ombe mwenye jicho moja, ng'ombe mwenye vichwa viwili na ng'ombe mwenye miguu mitano, lakini kwa mara ya kwanza ndio nimekutana na kiumbe kama hiki", alisema afisa mifugo huyo mwenye umri wa miaka 29.

Kichanga hicho cha kondoo kina macho, pua na mdomo kama binadamu isipokuwa masikio ndio ya kondoo.

Wataalamu wa mifugo wanafanya uchunguzi kujua chanzo cha kondoo huyo kuzaliwa akiwa na sura kama ya binadamu.

Mwezi septemba mwaka jana, mbuzi mmoja nchini Zimbwabwe alizaa kichanga cha mbuzi kikiwa na kichwa kama cha binadamu.

Kichanga hicho cha mbuzi kilikuwa hai kwa masaa kadhaa kabla ya wanakijiji waliotishika na sura yake kuamua kukiua.

Gavana wa jimbo alilozaliwa kichanga hicho cha mbuzi alisema kuwa mbuzi huyo alizaliwa kufuatia matunda ya uhusiano usiofaa kati ya mbuzi mwanamke na binadamu.


source.nifahamishe.com

Leave a Reply