WATOTO wanne wa mtaa mmoja wamekufa kutokana na kifo cha maji baada ya watoto hao kutoroka majumbani mwao na kwenda bichi kuogelea na kifo kuwakuta huko.
Watoto hao majirani wameacha simanzi na vilio kutawala katika eneo la Jangwani Mchikichini jijini Dar es Salaam kutokana na watoto hao wanne majirani kufa maji ka pamoja wakati walipokwenda kuogelea.
Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari jijini jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Bw.Liberatus Sabasi, alisema kuwa maiti za watoto hao ziliokotwa juzi majira ya saa 11 jioni, ufukweni mwa Bahari ya Hindi, eneo la Bomba la Maji Machafu, Feri Temeke.
Alisema watoto hao wote kwa pamoja walitoweka nyumbani kwa wazazi wao Januari 16 na kupatana waende kuogelea baharini.
Alisema kuwa baada ya kuogelea watoto hao walizidiwa na maji kisha kufariki dunia ambapo miili yao ilikutwa jana karibu na bomba la maji machafu.
Watoto hao ni Seleman Abdalah (11), Muhsin Salim (9), Abeid Salum (8- 9) na Abubakar Mohamed (8-9), wote wakazi wa Jangwani Mchikichini
Alisema uchunguzi wa kina utafanyika na baada ya hapo watoto hao watazikwa pamoja makaburi ya Ilala Kota jijini.
Katika tukio jingine Mwanamke aliyetamabulika kwa jina la Zaitun Waziri (28), mkazi wa Vijibweni CCM, amekutwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia mtandio wake alioutundika kwenye mti.
Kamanda Sabasi alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana saa 3 usiku, huko Vijibweni karibu na Shule ya Msingi Vijibweni.
Alisema kiwiliwili cha mwanamke huyo kilikutwa kikining'inia juu ya mti ambapo mwanamke huyo hakuweza kuacha ujumbe wowote uliomsababisha afanye hivyo.
Maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Temeke na polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.
source.nifahamishe.
Categories: