Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Ajiua baada ya kumchinja mkewe kwa wivu

-
Rehema Mwinyi.

MKAZI wa Kitefu wilayani Arumeru mkoani hapa, George Lukas (27), anatuhumiwa kumuua mkewe kwa kumchinja na kisu na kisha kuacha ujumbe mzito, kabla naye kujiua kwa sumu kutokana na wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Basilio Matei alisema tukio la kuuawa kwa mke huyo, Asumin Hussein (36), limetokea juzi saa 12 jioni katika Kitongoji cha Kitefu, Maroroni wilayani Arumeru.

Akielezea chanzo cha tukio hilo, Kamanda Matei alisema wanandoa hao wamekuwa na ugomvi wa mara kwa mara, huku mume akimtuhumu mkewe kuwa sio mwaminifu kwani amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine, na kwamba amewahi kutoa ujauzito wake ili aolewe na mwanamume mwingine.

Alisema siku ya tukio, mwanamume huyo alifika nyumbani na kuanza kudai ujauzito wake kutokana na majibizano, kulitokea ugomvi wa kutoelewana, na kusababisha mume kuchukua kisu na kumchinja mkewe, na kusababisha kifo cha mwanamke huyo.

Baada ya tukio hilo, Kamanda alisema Lukas alichukua karatasi na kuandika ujumbe kabla ya kujiua kwa sumu, ambayo haikufahamika.

Polisi baada ya kupata taarifa, walifika eneo la tukio na kukuta karatasi yenye ujumbe uliosomeka kuwa “nimeamua kumuua mke wangu kwa sababu ametoa mimba yangu na ana uhusiano na mwanamume mwingine.’’

Katika tukio jingine, Lembrisi Taiko (25), mkazi wa Sanawari Moivo katika Manispaa ya Arusha, ameuawa kwa kukatwakatwa na panga na wananchi baada ya kujeruhi kwa panga.

Kamanda Matei alisema tukio hilo limetokea juzi saa 4:30 usiku baada ya Taiko kukutwa akimshambulia kwa panga, Saimoni Lizer (45) na kumjeruhi vibaya kwa sababu ambazo hazikufahamika.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi.

Leave a Reply