Uvumi ulioenea nchini ya kwamba Maalim Seif emefariki dunia unaonekana hauna ukweli wowote baada ya kuthibitika kwamba Maalim anaendela vizuri katika Hospitali ya Hindu Mandal.
Uvumi huo uliokua ukisambazwa leo hii kwa njia ya simu (SMS)unaeleza kua Maalim Seif amefariki dunia leo katika Hospitali ya Hindu Mandal ambapo alikua amelazwa tokea jana baada ya kuanguka jana Uwanja wa Ndege Jijini Dar-es-salaam alipokua akisubiri ndege kuelekea nchini Oman.
Maalim alikua anasumbuliwa na tatizo la Presha pamoja sukari, lakini kwa sasa anaendelea vizuri na anatarajia kuruhsiwa kwenda nyumbani hii leo.
InshaaAllah Mungu ampe afya njema......Amiin
Categories: