Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Maiti ya mtoto yakutwa juu ya kaburi!!!

-
Rehema Mwinyi.


MAITI ya mtoto mdogo wa kike anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili hadi mitatu, imekutwa juu ya kaburi katika eneo la Buguruni Madenge, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema maiti huyo ambaye hajatambuliwa, aliokotwa juzi saa 5 asubuhi.
Alisema mwili wa mtoto huyo uliokotwa ukiwa hauna jeraha lolote, ingawa alikuwa anatokwa na povu mdomoni na kwamba mpaka sasa haijajulikana maiti huyo alifikaje juu ya kaburi hilo na kwa madhumuni gani.
Aidha, Kamanda Shilogile alisema sababu na chanzo cha kifo cha mtoto huyo hakijafahamika na maiti amehifadhiwa Hospitali ya Amana kwa uchunguzi zaidi huku Polisi ikiendelea na msako dhidi ya watuhumiwa.
Akizungumza kwa simu jana kufafanua tukio hilo, Kamanda Shilogile alisema hawajamkamata mtu yeyote kuhusiana na tukio hilo ambalo lina utata. “Mtoto alikuwa amefunikwa kwa nguo.
Hakuwa na jeraha lolote. Lakini unaweza kujiuliza maswali mengi kuhusu tukio zima. Je, alitupwa hapo? Alikuwa anaumwa, au ilikuwaje,” alisema Kamanda Shilogile na kuongeza kwamba hata mazingira ya kulihusisha na ushirikina, pia inawezekana.

Leave a Reply