gari linaloonekana ndio lilikuwa gari la Prez wa kwanza wa Zanzibar Marehemu A.Karume.
Milango ya Zanzibar ilianza kutumika katika miaka ya 1870 na kupata umaarufu mkubwa hadi sasa.Milango hii ilibuniwa na kuchongwa kufuatana na tamaduni za kihindi na kiarabu.
Katika miaka hiyo ya 18' jumla ya milango 806 ilitengenezwa. Hiki kilikuwa ni kipindi cha Sultan Bargash.
Katika miaka hiyo ya 18' jumla ya milango 806 ilitengenezwa. Hiki kilikuwa ni kipindi cha Sultan Bargash.
Sifa kubwa ya milango hii ni mapambo yake ambayo yalitokana na dhana ya kujikinga na madhara ya kishetani kuingia ndani ya nyumba. Mapambo mengine yaliyomo kwenye milango hiyo ni maua, matawi ya minazi, aya za Koran, jina la mwenye nyumba na mwaka uliotengenezwa mlango huo.
Zaidi baadhi ya milango hiyo imetiwa vyuma umbo la koni nyenye ncha kali ikiwa ni kama silaha ya kujikinga na uvamizi wa Tembo.
Zaidi baadhi ya milango hiyo imetiwa vyuma umbo la koni nyenye ncha kali ikiwa ni kama silaha ya kujikinga na uvamizi wa Tembo.
Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe, inastahili kupongezwa kwa kuhakikisha kuwa aina hii ya milango inaendelea kutumika katika Mji Mkongwe. Hii ni kutokana na kuwepo na wimbi kubwa la kung'olewa kwa milango hiyo katika miaka ya 80 kwa lengo la kuuzwa. Adhia kuwepo kwa ubadilishaji wa milango hiyo kutokana na kufanyiwa matengenezo ya nyumba.
picha na habari kutoka:kibunango.blogspot.com