Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

WANAFUNZI WA KITANZANIA NUSURA KUUWAWA KWA MOTO BANGALORE -INDIA

-
Rehema Mwinyi.


TANZANIA STUDENTS ASSOCIATION BANGALORE
(TASABA)
WANAFUNZI WA KITANZANIA NUSURA
KUUWAWA KWA MOTO BANGALORE -INDIA
-----------
Tarehe 11/03/2010 majira ya saa 11:30 wanafunzi wawili ,Hamis Mbelwa Fintan mwenye na Olais Alexendra Siarra waliokuwa wanakaa No.1093/1.11th Cross,Swarnanagar,Robertsonpet,KGF-563 122. Walinusurika kuuwawa kwa moto baada ya fujo iliyofanywa na wahindi wakidai kuwachukia waAfrika.
Wahindi hao waliamua kuchukua mafuta ya petrol na kumwaga dirishani na mlangoni, walifanikiwa kuwasha moto kupitia malangoni na moto kuanza kuingia ndani wakati vijana hao wakiwa ndani. Kwa bahati nzuri walifanikiwa kuuzima moto uliokuwa unaingia ndani na ule wa nje wasamalia wema waliuzima, bahati nzuri petrol ilikuwa chache hivyo hakuna madhara makubwa yaliyotokea.

Nilipopata taarifa hii nilitoka na kufika kituo cha Police cha Hennur Cross, nilitoa taarifa hiyo wakatoka maafisa wa police na kufika sehemu ya tukio wakati huo mimi nikiwa nimebaki kituoni. Baada ya dakika 30 police walirudi bila watuhumiwa, nilipouliza walinijibu nirudi nyumbani wameshawatuliza na hawatarudia tena nilibishana sana na police juu ya hilo maana walipofika waliwakuta watuhumiwa na kuwaachia waende huru.
Nilizidi kupigania haki lakini walinijibu “This is India not Tanzania and we have to cop with them like it or not” niliwauliza kama huo ndio utamaduni wao wa kumwagia watu petrol na kuchoma moto kutaka kuwaua? Wakasema kama naona hawajanisaidia niende kutafuta msaada mahali pengine.
Nilisikitika sana kwa kauli za police hasa ukizingatia kuwa toka kifo cha mwenzetu Imran Mtui ni mwezi tu na siku 7 mpaka sasa na hatujapata taarifa ya kuridhisha kutoka kwa police halafu linatokea jaribio lingine la kuua kwa kutumia petrol.
Hali hii inatisha hasa nikiwa kama mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi kuona raia wenzangu wanatishiwa kutolewa maisha yao kwa moto na bila hatia huku police wakiona jambo hilo ni la kawaida kwao na kuwaachia watuhumiwa waende huru. Watu hawa wanaishi nchini kwetu kwa amani na kufaidi matunda ya uhuru na uchumi wa nchi yetu bila bugudha.


Baada ya kuona hakuna masaada kutoka police niliwashauri Hamis Mbelwa Fintan na Olais Alexendra Siarra wahame mahali pale kwani hapana usalama tena. Tunaomba sana msaada toka nyumabani na ofisi zetu za ubalozi zilizopo New-Delhi India kutafuta jinsi ya kufanya waTanzania waishio Bangalore –India na kwingine kote kuishi kwa amani, imezoeleka kuwa mara zote wanafunzi ni wakorofi lakini kwa tukio hili nakataa kabisa kama chanzo ni wahanga hawa bali ni chuki binafsi iliyoko dhidi ya wa Afrika ambayo inatufanya tuishi kwa uoga na wasiwasi mkubwa sana. Leo hii petrol ilikuwa chache siku nyingine itakuaje? Je wangefanikiwa kutoa roho za vijana hawa majibu kutoka vyombo vya dola vya India ingekuwa ni nini? Au wangesema wamejiua tena vijana hawa kwa moto? Haya ni maswali machache ya kujiuliza.


“Mungu ibariki Tanzania, Mungu tubariki wanafunzi wa kiTanzania tuishio Bangalore India”


Fidelis Msomekela


Mwenyekiti – TASABA

+919742176980

Leave a Reply