KIJANA Mtanzania aliyeingia uwanjani na kwenda moja kwa moja kumkumbatia kiungo nyota wa Brazil, Ricardo Kaka amekuwa gumzo na ‘shujaa’ kwa mashabiki wa soka nchini.
Kijana huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja aliingia uwanjani wakati mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars na Brazil inaendelea na kwenda kumkumbatia Kaka.
Mashabiki walionyesha kuvutiwa naye na kuanza kumshangilia kwa nguvu, kama hiyo haitoshi mashabiki uwanjani hapo waliwazomea askari Polisi walipoanza kumpiga wakitaka wasifanye hivyo.
”Wale askari hawajui mapenzi, yule kaonyesha ustaarabu, kamkumbatia Kaka halafu katoka zake uwanjani wala hajafanya kitu chochote. Anastahili sifa,” alisema shabiki mmoja akiunga mkono na wenzake ambao waliendelea kuwazomea askari Polisi.
Hata baada ya mechi kijana huyo ambaye alikamatwa na Askari Polisi alikuwa gumzo kubwa huku watu wengi wakimpongeza kwamba ametimiza ndogo yake kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kumkumbatia Kaka tena katikati ya uwanja lakini kwa amani ya kutosha.
Kijana huyo alitokea Magharibi ya uwanja huo na aliruka uzio baada ya kuvua viatu na kutoa kila kitu alichonacho mfukoni akihofia kuonekana anakwenda kumdhuru Kaka.
Baada ya hapo alianza kuingia uwanjani akiita, “Kaka, Kaka, Kaka”, huku akionyesha kama anataka kulia. Baada tu ya kumfikia, alimkumbatia kama mtu wanayefahamiana siku nyingi, Kaka hakuwa na hiyana alimpokea vizuri.
Halafu Kaka anayechezea Real Madrid, alimuomba shabiki huyo atoke uwanjani ili waendelee kusukuma gozi, naye taratibuu alitoke nje upande wa Magharibi kama mtu aliyefunga bao, mikono juu na mwenye furaha.
Waliokuwa wamekaa naye karibu walieleza kuwa kijana huyo alifanya maandalizi ya takribani dakika 15 akijiandaa kuingia uwanjani na mwisho aliapa, “potelea mbali kama nitafungwa au nife sawa, mimi naenda kwa Kaka.”
Kupata picha zaidi za tukio hilo bonyeza hii 'Link' hapa chini
http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/jamaa-aweka-histori...
habari kwa hisani ya global publishers
Categories:
nimependa ushujaa wake, jamaa kakamilisha ndoto zake, bila kujali kipi kitatokea!
na ndivyo inavyotakiwa kila siku...wacha tumuite shujaa maana tupo wengi tunaotamani hata kumshika ila tumeshindwa.