Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

MTANZANIA AFUNGWA MAISHA MAREKANI!!!!

-
Rehema Mwinyi.


Mfungwa wa kwanza katika jela ya Guantanamo kushtakiwa kwenye mahakama ya kiraia, Ahmed Ghailani kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama ya jimbo la Manhattan.

Ghailani alipatikana bila hatia mwaka jana, katika kesi ambayo alishtakiwa kwa mauaji pamoja na mashtaka mengine kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 1998 katika balozi za Marekani mjini Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania


Mchoro ukionyesha Mtanzania Ahmed Ghailani

Jopo la majaji hata hivyo limempata na hatia ya kufanya njama ya kuharibu majengo ya serikali.

Upande wa mashtaka ulijaribu kumshawishi jaji kwamba Ghailani alipaswa kuonewa huruma kwa sababu hakujua kuhusu njama hiyo.

Vile vile walisema kuwa Ghailani aliteswa na CIA baada ya kukamatwa.

Hata hivyo waendesha mashtaka walitaka apewe kifungo cha maisha gerezani huku wakisisitiza kuwa alijua kuhusu njama hiyo.

Akijiandaa kutoa hukumu yake, Lewis A. Kaplan alisema ilikuwa siku ya haki kwa jamii za watu 224 waliofariki kwenye mashambulizi ya bomu ya mwaka wa 1998 pamoja na wale wote waliojeruhiwa.

Kaplan alisema aliridhishwa na ushahidi aliopata kwamba Ghailani alijua kwamba watu wangekufa kutokana na vitendo vyake.

Ghailani alikamatwa nchini Pakistan mwaka 2004.

Alipelekwa kwenye kambi ya siri inayosimamiwa na shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, kabla ya kupelekwa Guantanamo Bay, Cuba, mwaka 2006.

Baadaye alihamishwa hadi New York alikoshtakiwa.
Credit to BBC.

Leave a Reply