Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

WEWE NI MWANAMKE/MSICHANA NA UNAENDESHA GARI,UNAPASWA KUJUA YAFUATAYO....

-
Rehema Mwinyi.


Sasa hivi wanawake/wasichana wengi ni madereva...wanaendesha magari sana tu tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo wanaume ndio walikuwa wengi wana magari na wanaendesha magari.
Wanawake sisi tumeshajiwekea kichwani kwamba sisi tunaendesha tu gari na kazi yetu ni kuweka mafuta tu kwenye gari(petrol/deasel) basi.Au kuhakikisha gari safi lakini mengine ni kazi ya wanaume...sio kweli kuna vitu ambavyo unapaswa kuvifaham kuhusu magari.
Kubadili Tyre
unaweza kuwa sehemu ambayo hakuna hata mtu wa kuku saidia halafu tyre imepata pancha.Kwenye gari una jeki,spana na spair tyre lakini kubadilisha Tyre huwezi.Jifunze hili wala sio kazi mimi sio dereva lakini nimeshawahi kutoa tyre na kuweka tyre inasaidia sana hata gari ikikuhabibikia mahali unakuwa huna wasiwasi na kuanza kusumbua watu.
Kuweka maji ya wiper
Wakati mwingine vioo vimepata uchafu,vumbi,kioo kimenyewa na ndege,...unataka kusafisha lakini hakuna maji ya kwenye wiper na wala hujui yanawekwaje.Unapaswa kujua hili ni kwa manufaa yako mwenyewe binafsi.
Pia unapaswa kujua kuweka oil kwenye gari lako na hata namna ya kuicheki kabla hujaweka.
Break down
Gari inaweza kupata tatizo ikashindwa kuwaka kabisa,kuwa na namba za watu wa break down kabisaa ili kikinuka basi unapiga simu ili uje kutolewa hapo ulipoharibikiwa na gari.

Hivi ni baadhi na muhimu uavyoweza kujua ili hata jambo likitokea basi huna wasiwasi kivile kisa hujui pa kuanzia.

source dina marios

Leave a Reply