Sharing this story may save some life,may touch someone's life in a similar related problem,may bring hope to hopeless situation.yawezakua si wewe na unaweza kuchukulia just simple.ila yaweza kumgusa mwenzio na kupelekea ku save maisha yake..
tumekua tukiamka kila leo na kutembea , unaweza kujiona una nguvu na afya tele bila ya kujijua kuwa kuna ugongwa unakula ndani kwa ndani,
au unaweza kutokewa na hali isiyoya kawaida ya hafla ila ukapuuzia na kuipa kisogo,waweza kugundua tatizo kwa mtoto wako ndugu yako,jirani yako au mtu yeyote
yule wa karibu bali ukajenga woga au ukazarau na kutokutilia manane hali yake,bila ya kujua kuwa ukimya wako unazidi kuhatarisha maisha ya mwenzako huyo.
kila kiungo kina u.muhimu katika mwili wa binaadamu ila siku ya leo napenda kugusia zaidi kwenye Macho.
CONE SHAPE YA CORNEA
KERATOSCONUS
ni jina kutoka Greek na ni miongoni mwa magojwa ya macho.na naweza kuitafsiri kama hali ya kuendelea ambayo inafanya muundo wa kawaida
wa cornea ambao ni curve kwenda kwenye muundo wa cone.
ukijiuliza chanzo au sababu ya maradhi haya jibu ni kuwa hakijulikani ingawa wana sayansi wamejaribu kuleta vyanzo tofauti.
wapo wanaosema ni urithi na mazingira yanachangia.keratoconus huathiri mtu mmoja kwenye watu zaidi ya 2000.ingawa kwa hivi sasa maradhi haya yanakua zaidi.
back to my story nilipokua na umri wa miaka 4 nilianza kupata tatizo la macho na baada ya kupelekwa hospital nilishauriwa kuanza kutumia miwani
jambo hili halikuungwa mkono na mama angu na ikambidi ajaribu kutafuta njia na ushauri kutoka kwa madaktari mbalimbali..na ndipo aliposhauri badala ya kuvaa miwani nijaribu kutumia tiba mbalimbali na vyakula vitakavyonisaidi hadi umri wangu utakaposogea mbele
nilipofika std 5 hakukuwa na jinsi tena bali ni kurudi hospital na kuanza kuvaa miwani kwani tayari macho yangu yalishaanza kupoteza uwezo wa kuona bila ya masaada huo.
sikuwa napenda kuvaa miwani kwani yalikua yakinikosesha raha na kunizuia kushiriki katika michezo mbalimbali shuleni na badala ya takecare of myself inanibidi ni takecare of my glasses,haikua rahisi.
niliendelea kubadilisha miwani muda baada ya muda na kila siku ninapo kwenda kupima namba zangu zikawa zinabadilika.
sikutilia manani kwasababu sikuwa na elimu yeyote juu ya maradhi haya ya macho.inapotokea siku sioni tena basi ninachofanya ni kupima mawani mengine.
hali iliendelea kuwa hivyo na ikafikia wakati hata nikipima nakosa kipimo sahihi cha namba yangu. maisha niliyaona magumu sana kila unapofika muda wa shule maana hata ninapoingia darasani inanibidi kuchungulia daftari la jirani pindi mwalimu anapo andika notes na pale anapofahamisha inanibidi nimsikilize tu bila ya kuona anachoandika.
na ikawa inanibidi kutumia nguvu za ziada kuyalazimisha macho kuona kilichoandikwa ubaoni na hapo ndipo inapopelekea maumivu makali ya kichwa.kuishi na Keratoconus haikua rahisi kwangu kipindi chote cha elimu ya secondary kwanza nimekua nikiishi na ugonjwa
MUONO WA MTU MWENYE KERATOCONUS
nisioufahamu na pili wanafunzi wengi darasani wamekua wakinicheka pale ninaposhindwa kuandika na kukosa kuona kilichoandikwa ubaoni labda ni akili zao za kitoto au ni kutokuelewa kwao ila uwepo wa tabia yao hii mbaya ulikua ukinikosesha raha sana na ukiathiri maendeleo yangu,nikawa nachukia sana kufika shule.
2007 nilibahatika kwenda hospital kubwa ya macho kwa lengo la kutaka kupatiwa miwani.lakini sikuamini na nilihizunika sana nilipoambiwa huwezi kupata namba yako sahihi bali ni kutumia contact lens na ni ngumu sio soft one.
CONTACT LENS
kwa bahati mbaya hospitali hapo licha ya kuhoji na kuwa na shauku ya kutaka kujua tatazi langu sikuelezwa nini hasa kisayansi zaidi bali ni kuambiwa kuwa cornea yangu imebadilika shape,laiti kama ningeelezwa kiundani zaidi tangu kipindi kile ingesaidia sana na kuniokoa, tatizo limekua likikua siku hadi siku.. nilibahatika kununua contact lens na kuanza kutumia..
CONTACT LENS
iliniwia vigumu mno kuzoea hali ile ya kila ufikapo asubuhi badala ya kuwahi darasani wewe uhangaike kuvaa lens.na kutokana na hali ya hewa ya vumbi
inanilazimu kuzivua kila mara ninapoingia mchanga machoni.baada ya miezi kadhaa ya uvaaji wa contact lens ikanilazimu kuacha na kurudia tena kwenye miwani yangu ingawa sikuwa naona vizuri
2008.nchini india nilifanikiwa kupata namba sahihi ya miwani na nikaanza kutumia. ila namba hiyo imekua ikibadilika siku hadi siku.nimekua nikipata namba tofauti kila ninapo tembelea hospital kwa vipimo.
2010, mwanzoni doctor akanishauri nifanye lasik eye surgery au kwa jina jengine tunaita laser treatment.tiba hii husaidia kurudisha vision yako na kupelekea ww kutokuvaa miwani tena.nilifarijika baada ya kusikia kuwa nitaweza ishi bila ya kuvaa miwani nikaendelea kujipa tamaa na kuendelea kuchanga pesa kwa ajili ya tiba hii..kipindi hichi chote sikugundua mabadiliko makubwa ila hadi pale ninapopima miwani mapya.mabadiliko hutoke kwenye namba.
JUNE 2011 zanzibar ndipo niligundua kuwa vision imebadilika kwasababu sikuwa na uwezo tena wa kuona vizuri bila ya miwani,kila nilipojaribu kuvua miwani nilichokua naona ni blurred.baada ya kuona mabadiliko haya nilikua siamini na nilikua nikilia every second ninapovua miwani na ikawa inanilazimu
kushinda na miwani siku nzima kila sehemu.niliogopa sana na ku hofia naweza kukosa uwezo wa kuona..
MUONO WA MTU MWENYE KERATOCONUS
MUONO WA MTU MWENYE KERATOCONUS
July 2011,Namshukuru Mwenyezi mungu kwa kunipa akili ya kufikiria kwenda hospital kwa ajili ya kufanya lasik treatment,Pia namshukuru sana my dearest friend kwa kunipa moyo na kunishawishi kufanya hivi.Sushrutha eye hosptal chini ya Dk Pallavi ni hospital nzuri ya macho na inayoaminika..nikaamini kuwa pale nitapata tiba ya tatizo langu.
na baada ya Dk kuniona akanieleza nije siku ya pili mapema kwa ajili ya vipimo.
July 15 2011.mapema asubuhi nilifika hospital na baada ya muda nikaona na Dk na kuanza vipimo kama alivyoniahidi..nilitumia nusu siku kwa ajili ya vipimo.na alichoniomba niwe msatahamilivu kwani macho ni kitu hatari sana na huwezi kukurupuka tu kwa kuchukua vipimo juu juu bali wanachotakiwa ni kurudia vipimo
na hadi kuhakikisha majibu waliopata ni sawa.nilimaliza vipimo vidogo na kwenda kumalizia na kipimo kinachoitwa orbscan .na ndicho kilichoonesha kuwa nina Keratoconius..
nilishindwa kujizuia nilianza kulia sana nilifikiria mambo mengi sana itakuaje baadae?je vipi kama hii hali ya kuchongeka kwa cornea haijasita what will happen after?
baada ya muda Pallavi Dk akanipatia njia pekee ambayo natakiwa kufanya na sio nyengineyo bali ni C3-R (corneal collagen cross-linking riboflavin) hii ni aina ya tiba ambayo anatakiwa kufanyiwa mgonjwa wa keratoconus ambae ameshatumia both classes and contact lens na kushindikana.
na sasa nipo kwenye process ya kutaka kufanya hii treatment miezi michache ijayo kabla hali haijawa mbaya zaidi..
MPENDWA MSOMAJI
Nimetoa mfano wa keratoconus sina maana ya kuwazungumzia wenye hili tatizo tu bali nina maana ya kuwafumbua na kuwaambia muwe makini na afya zenu na mmpendelee kuangalia afya zenu na msisubiri hadi tatizo liwe kubwa
na haliwezi kutibika tena.Tujaribu kujipenda na kujijali sisi wenyewe na pia tuelewe kuwa hakuna mtu atakae kuja kukushika mkono na kukuambia twende checkup ya tumbo or cancer na kadhalika.Ni wengi sana miongoni mwetu wameweza kuokoa afya zao baada ya kuona mabadiliko wamekimbilia hospital na baada y
a vipimo anaambiwa ni cancer inaanza ila tunaweza iwahi na ukapoa..Bado hujachelea,Bado una muda wa kuwahi afya yako,bado una muda wa kuchunguza afya yako,fanya hivyo leo na usingoje kesho,na tumia muda wako kumuelesha mwenzio na usijali jinsi gani
atapokea ushauri wako.
Remember Inspire Me
Daily.One Person Can Make a Difference.You can change someone life.
Happy birthday to me.
Thank you for sharing this Abdul. I am a Keratoconus patient as well. One eye is blind, in spite of cornear transplant at KCMC. The surgery went extremely well, but had lost the use of my eye because it was non-functioning for many years and became dormant. This situation is irreversible. Your point of having regular eye check-ups makes a lot of sense. Had my parents done this, I could be having perfect sight today. Thanks to Dr Janna and a German doctor know as Michael (this is 20 years ago now, I do not think they are still at KCMC today?). I tried to get C3-R in London, but the law is against such a procedure to a patient with only one functioning eye. I am disappointed because of that, but thank God I can still see well with my one functioning eye even though it is also Keratoconus laden. If you want to contact me and share more about Keratoconus, use this email: 47975105@mylife.unisa.ac.za
Mmmh Pole sana mpendwa na Mungu atazidi kukuponya,pia ahsante sana kwa ujumbe mzuri na wakufundisha,Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa na Mola akuongezee mingine mingi.
Thank you very much for sharing this!
Nice of you to share-- had to read because i too have eye problems--that i tend not to care tooo much,i have glasses but i dont put on all the time,i just can see far!
Ahsante sana swahili na waswahili..
August 25, 2011 7:35 PM
tafadhali nakushauri sana ulitilie mkazo suala hili na ujue na ujaribu kutumia miwani hayo kama ulivyoambiwa na daktar..kwa kufanya hivyo yaweza kukusaidia bado mapema.mm binafsi mwanzo nilizani tu siwezi kuona mbali kumbe nilikua na tatizo hili..
thnx Anonymous wa August 25, 2011 1:00 PM
kwa ku share nasi tatizo lako pia..we will be in touch soon..thnx
Real inspiring cause i've the same problem,mpk nishajikatia tamaa kbs ya kuwa nisipopata pesa ya kwenda kutibiwa India ndio bac tena!!
Hi
Nice info, worth sharing. Where is this hospital? Plz respond to wwwdotjj@yahoo.com
thnx richard na pole sana unachotakiwa ni kutokata tamaa na kuamini ipo siku kila kitu kitakuwa fine..na naomba nikutoe woga wa kuona india matibabu ni ghali hapana matibabu sio ghali kama tunavyofikiria wengi wetu.
thnx, hii hospital ipo nchini india..if you need help or more info plz am here to help you ili kutatua tatizo lako.thnx
Richard, je umejaribu KCMC? Mdogo wangu ana Keratoconus macho yote mawili na alifanyiwa operation ya cornear transplant KCMC. Sasa anaona vizuri sana. Pia kuna hospitali nyingine Nairobi sehemu ya Thogoto inaitwa Kikuyu hospital. Wanafanya cornear transplant viruzi sana. Hauhitaji appointment, unakwenda tu na kukaa kwenye foleni. Utaonwa na daktari na ukionekana unahitaji transplant watakupatia appointment siku ambayo wanategemea kupata cornears kutoka UK. Mimi ilinilazimu nisubiri donor KCMC kwa kulazwa hospitalini miezi minne kwa sababu lazima awe kijana na asiwe na virusi vya ukimwi (wanachukua graft cornear kutoka kwenye maiti). Ndiyo maisha, Mungu atakusaidia. Kama unauwezo, nenda UK. Kuna watu wanajiita accuvision http://www.accuvision.co.uk/. Shida yao tu ni kwamba wanachaji pesa nyingi sana, angalia tu kwenye website yao. Ukitaka namba ya dada yangu niambie tu nitakupatia.
Thanx Abdul &Mr,Anonymous 4very couraging comments to me. U real inspire me this mornimg and see a bright future 4my eyes. Let me leave my e-mail 2u for me to get close contact with you all. E-mail:rfmndolwa@yahoo.com
Be blessed all
welcm richard..ila kupitia hapa hapa ningependa kuwashauri wale wote ambao wana plan ya kufanya hii cornea transplant hii ni solution ya mwisho kabisa ya tatizo hili..na plz kabla hujafikiria kufanya hii muulize dk wako juu ya C3R which means Collagen Crosslinking using Riboflavin.after few days ntakuja na makala juu ya hii treatment..thnx
Abdul, nakushukuru sana kwa point hiyo. Kweli Cornea transplant ni solution ya mwisho. Shida ya familia yangu ilikuwa ni umaskini. Hatukuweza kughalimia ghalama za matibabu tofauti nje ya Tanzania. Halafu C3R ni tiba ya hivi karibuni sana. Ahsante sana kwa kuweka point hiyo muhimu. Ila kama nilivyosema, mimi C3R imekataliwa kwa sababu ninajicho moja tu linaloona na sheria ya UK (nilikukwenda kwa matibabu) inakataa kufanya C3R kama kwenye jicho peekee linaloona.Ninamshukuru Mungu bado hali si mbaya sana kwa sasa na nimekwisha vuka miaka 30 (wanasema ukifikisha miaka 30 uwezekano wa Keratoconus kuendelea kukua ni chini ya asilimia 2). Kama nitazidiwa (which is very unlikely) itanibidi nitafute matibabu India au South Africa. Daktari wa UK alisema inaghalimu kama Dola 1500 kwa kila jicho. Nadhani bei zinatofautiana kulingana na hospitali, ni kama vile bei zilivyo tofauti kati ya Aghakhani Hospital na Hindu Mandal. Link hizi zinaweza kusaidia kwa utafiti zaidi:
http://www.lasikindia.in/c3r_topoguidedprk.htm
http://www.5min.com/Video/Explaining-the-C3-R-Procedure-326746699
Thanx Abdul 4advice,waiting 4that makala!
c3r nchini india ni dola 1000 kwa macho yote mawili..pamoja na dawa.