Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Watu 36 Wauliwa Kwa Kupigwa Risasi Baa

-
Rehema Mwinyi.

Zaidi ya watu 36 wamefariki dunia nchini Burundi baada ya watu waliokuwa na silaha kuvamia baa na kuwapiga risasi watu wote waliokuwemo kwenye baa hiyo Watu 36 wameiaga dunia huku wengine wakiwa wamelazwa hospitali hali zao zikiwa mbaya baada ya watu waliokuwa na silaha kuvamia baada moja iliyopo nje kidogo ya mji mkuu wa Burundi, Bunjumbura na kuwamiminia risasi watu wote waliokuwemo kwenye baa hiyo.

Tukio hilo lilitokea jana wakati kundi la watu wanaoaminika kuwa ni waasi wa Burundi wanaoishi nchini Kongo kuvuka mpaka na kuivamia baa hiyo iliyopo kwenye mji wa Gatumba.

Gavana wa Bunjumbura, Jacques Minani alisema kuwa watu waliofanya shambulio hilo waliingia Gatumba baada ya kuvuka mto wakitokea nchini Jamhuri ya Kongo.

Mmoja wa watu waliojeruhiwa kwenye shambulio ambaye alipigwa risasi ya tumbo, alisema kuwa watu waliofanya shambulio hilo walikuwa wamevaa nguo za kijeshi.

"Mmoja wao alisema Waue wote waue wote hakikisha hakuna atakayenusurika", alisema majeruhi huyo aliyejulikana kwa jina la Jackson Kabura.

Kundi kubwa la watu waliokuwa na silaha nzito za kivita waliivamia baa inayojulikana kwa jina la 'Chez les Amis' na kuwalazimisha watu wote walale chini.

Mwanaume mmoja ambaye alinusurika maisha yake ingawa ndugu zake wawili waliuawa kwenye shambulio hilo alisema kuwa "Walimwambia kila mtu alale chini na ndipo walipoanza kupiga risasi."

Miili ya watu iliachwa kwenye maegesho ya magari katika hospitali moja mjini Gatumba huku taarifa zaidi zikisema kuwa idadi ya majeruhi imekuwa kubwa kuliko uwezo wa hospitali.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi aliahirisha safari yake ya kwenda New York, Marekani na kutembelea eneo lilipofanyika shambulio hilo na kuahidi kuwachukulia hatua kali watu wote waliohusika.


na nifahamishe.

Leave a Reply