Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Sita Wafariki kwa Kula Kasa Micheweni

-
Rehema Mwinyi.

    WATU sita wamefariki dunia Tumbe wilaya ya Micheweni Pemba na wengine kulazwa hospitali wakiwa hali zao mbaya baada ya kudaiwa kula nyama ya kasa.

Taarifa kutoka kisiwani humo zinaeleza kuwa waliofariki katika mkasa huo wakiwemo watoto ni pamoja na Sara Hamad Bakar (55), Aisha Said Juma (7), Fatma Abdalla Rajab (5), Mariyamu Said Juma (5), Nasria
Khatib Haji (1) na Zuwaifa Omar Khamis (6).


Waliolazwa katika hospitali ya Chake Chake ni pamoja na Said Juma Khatib (45) ambaye ndiye mvuvi wa kasa huyo, Said Juma Khatib (20), Rehema Bakari Simba (25), Mwanakhamis Hamad Mwijab (70), Mkitu Haji Abeid (48) na Zaina Juma Khatib (22) ambaye ametibiwa na kuruhusiwa kutoka.

Kasa huyo alivuliwa kutoka baharini Januari 3 mwaka huu, ambapo baada kuchinjwa huko huko baharini alitengezezwa na kuletwa nyumbani kwa ajili ya kitoweo.

Habari kutoka Pemba zinaeleza kuwa baada ya kumla kasa huyo, iliwachukua saa 3 kuanza kupata athari za nyama yake kwa kuugua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Hemed alithibitisha tukio hilo na kuwataka wananchi waache ukaidi kwa kula nyama ya kasa.

Alisema wananchi wakiendelea na ukaidi kwa maagizo yanayotolewa ndipo madhara yanapojitokeza jambo ambali huathiri jamii.

Hadi jana watu watano maiti zao zilikwisha kabidhiwa kwa na kuzikwa na ndugu na jamaa zao.

Leave a Reply