Mnikulu Zanzibar afariki dunia
MNIKULU katika Ikulu ya Zanzibar, Shaaban Ahmada Hilika, amefariki dunia leo katika hospitali ya Mnazimmoja alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Hilika anatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Mfenesini baada ya Sala ya Adhuhuri, na mwili wa marehemu utaondokea Amani nyumbani kwao, baada ya kuagwa na kusaliwa..
Hilika amekuwa Mnikulu katika Ikulu ya Zanzibar tokea uongozi wa Aawamu ya Sita ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Dk.Amani Abeid Karume na kuteuliwa tena kushika nafasi hiyo na Rais wa Awamu ya Saba wa Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein.
Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu, Amin.
Ameen, inna lillah wainna ilayh rajiun.