Nilikua njiani naelekea ofisini kwangu, nikiwa mitaa ya Darajani Zanzibar simu yangu iliita aliyenipigia alijitambulisha na nilikua simjui, alisema yupo Mkoani Kigoma anafanya kazi shirika moja la kimataifa, alinieleza anahitaji mtu wa kushirikiana naye katika mambo ya kibiashara anayetoka Zanzibar, alidai alipatiwa namba yangu na moja kati ya rafiki zangu wanao ishi Uk, na hakutaka nimuulize niliendelea kumsikiliza.
Akaanza kunielekeza anafanya Biashara ya kununua Product ambayo inahifadhi vyakula visiharibike na akanipatia namba ya mtu anayehusika katika utengenezaji wa production na jina lake akadai anaitwa Ibrahim na anapatikana Mahonda Zanzibar, akaniambianimpigie Ibra kumuuliza kama hiyo Production ipo na inapatikana kwa bei gani, nilimpata Ibrahim na akanieleza wanazo bidhaa kutoka ncho tofauti lakini best zinatoka Sweeden na bei yake kwa chupa 2 ni T shs 1,200,000/= nikamjibu yule jamaa aliyenitambulisha kwa Ibra kwamba bei yake ndio hiyo, baada ya hapo akaniambia kwamba pia wapo mabosi wake wa kizungu wamefikia Zamani Kenpisky Hotel Pwani Mchangani wananunua hiyo bidhaa kwa bei ya juu sana mara 2 ya bei ya kununulia, wakati nawasiliana na hawa jamaa tokea dakika ya kwanza niligundua kwamba hawa ni matapeli na nilichukua hatua za kuripoti tukio hili kituo cha Polisi na walifika kwa wakati nikawa nawashirikisha katika mawasiliano na hawa matapeli.
Polisi niliwapatia namba za simu za hawa jamaa wakaweza kuzifanyia utafiti na wakagungua wenye kuzimiliki, na sasa baada ya muda mfupi nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwamba anaitwa Fred yupo Kenpsky na ameelekezwa kwangu kuja kununua Product mimi sikujivunga nikamwambia zitapatikana ndio hapo akaniambia kabla sijapeleka mzigo nimpelekee sample 1 pair ili akiridhika nao ndio tunaondoka pamoja na kwenda kuchukua mzigo wote.
Nikamweleza yule jamaa aliyenipigia simu mwanzoni kwamba wanunuzi wanahitaji sample wakiridhika ndio wanunue mzigo wote, hivyo akaniambia niwasiliane na Ibra kuhusu sample nikampigia akaniambia beio yake ndio hiyo aliyoniambia hapo juu Milioni moja na laki mbili, nikamjulisha jamaa akaniambia nifanye maarifa nipeleke hizo pesa.
Nikawaeleza Polisi tukaweka mtego baada ya muda kidogo nikawaambia kwamba fedha tayari waniletee mzigo, wakanielekeza walipo wakaniambia wapo Kibweni tukaenda mimi nilitangulia na polisi wakiwa nyumba yangu kwa umbali kidogo, nikapiga simu akaja kijana mmoja akaniuliza ni wewe niliyeagizwa kuhusu mzigo nikamwambia ni mimi na mzigo uko wapi nikupatioe hizo fedha? akaniambia nimsubiri kidogo akaufuate niliendelea kusubiri pale na kupiga simu hakutokea baadae alizima simu kabisa.
Nikawaarifu polisi kwamba jamaa wameshtuka nikarudi ofisini kwangu. nilichoamua kufanya baada ya hapo niliwapigia simu wale jamaa wote tuliokuwa tunawasiliana kwamba nawashukuru sana mzigo nimeupata na tumeshafanya biashara nimemkabidhi jamaa Milioni moja na Laki mbili ispokuwa jamaa aliyepokea pesa alitaka wale jamaa wote wasijue kama tayari ameshapokea fedha.
na nikawashukuru sana sikujua kilichoendelea baada ya hapo, hii ni tahadhari natoa kwa wenzangu wa JF na watanzania tuwe makini na tujiepushe na tamaa za kijinga tutaingizwa mjini.
nawasilisha.
Categories: