Lulu alipandishwa kizimbani kwa usiri mkubwa akitokea Kituo cha Polisi cha Oysterbay alikokuwa akishikiliwa na kupandishwa kizimbani moja kwa moja bila kuwekwa mahabusu ya mahakama hiyo kama iwavyo kwa washitakiwa wengine wanaosubiri kusomewa kesi zao.
Baada ya kupandishwa kizambani alisomewa shitaka lake na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Elizabeth Kaganda ambapo alisema Mnamo Aprili 7 mwaka huu majira ya saa saba za usiku maeneo ya Sinza Vatican jijini Dar es Salaam Elizabeth Michael (18) alimuua Steven Kanumba. Katika kesi hiyo mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote isipokuwa alinyoosha kidole na kupinga umri uliotajwa kuwa ana miaka 18 na kusema umri wake ni miaka 17. Baada ya kusomewa shitaka hilo, Lulu alipelekwa gerezani Segerea na kesi yake itasikilizwa tena aprili 23 mwaka huu.
source.GPL