Father Ambros Mkenda wa Kanisa la Katoliki la Mpendae amepigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake majira ya saa 12 jioni jana wakati akitokea kanisani. Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Azizi Juma amethibisha kutokea kwa tukio hilo na amesema hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusika na tukio hilo lakini uchunguzi unaendelea. Father Mkenda hivi sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo Askofu wa Anglikan Michael Hafidh amesema bado ni mapema mno kuelezea kama ataendelea kuwepo hospitalini hapo au atasafirishwa huku akilaani vitendo ambavyo hivi vinavyoendelea vya kuwahujumu viongozi wa dini.