Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Gas City: Hospitali ya Apollo kujengwa Kilwa

-
Rehema Mwinyi.


Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi na wakaazi wa mikoa ya kusini kwa ujumla, wanatarajia kunufaika na ugunduzi wa gesi katika visiwa vya Zafaran na Lavan vilivyopo wilayani huo. Kampuni ya Statoil kutoka nchini Norway ikishirikiana na Exxon Mobil imegundua gesi katika Visiwa vya Zafaran na Lavan vilivyopo Kitalu namba 2, Ukanda wa Pwani ya Tanzania, hususan Pwani ya Kilwa mkoani Lindi. Kutokana na ujio wa wageni hao, Watanzania hususan wakazi wa Kilwa, Lindi na Mtwara kwa jumla hawana budi kupata faida za moja kwa moja na zingine zisizo za moja kwa moja ikiwemo gesi hiyo kutumika kutengeneza umeme utakaopatikana kwa uhakika na kuuzwa kwa wananchi wote. 
Akizungumza mjini Kilwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilwa, Adoh Mapunda amesema kuwa, madiwani, watendaji na mkuu wa wilaya wamekaa na kutafakari kwa kina juu ya faida ya kudumu itakayoonekana wilayani humo kutokana na ujio wa mradi wa gesi. Amefafanua zaidi kuwa mradi huo ni ujenzi wa hospitali ya kimataifa itakayolingana na ile ya Apollo nchini India ambayo viongozi mbalimbali duniani hukimbilia kwenda kutibiwa ambayo itajengwa na mwekezaji na itaendeshwa na taasisi nyingine ya kimataifa huku halmashauri ikiwa na hisa za kupata gawiwo la kila mwaka kutokana na faida. Mpango huo unatekelezwa kupitia utaratibu uliopo katika mikataba kwa wawekezaji kuhusu uwajibikaji na ushiriki katika masuala ya kijamii. Amesema kuwa, tayari Statoil imetenga Sh18 bilioni kuanza ujenzi wa hospitali hiyo mjini Kilwa wakati wowote kuanzia mwaka huu ambapo michoro ya hospitali hiyo ipo tayari huku ikitarajia madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi na itakuwa na wafanyakazi wataalamu, pamoja na wahudumu ambao wengi watatoka Halmashauri ya Kilwa.

Leave a Reply