Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

RAIS JAKAYA KIKWETE AWASILI WASHINGTON DC‏


 Rais Dkt Jakaya Kiwete  akiingia Ritz Calton Hotel wakati alipowasili Washington, DC kwa kuendelea na ziara yake ya nchini Marekani aliyoanzia kwenye miji ya San Francisco na Vallejo, California.
 Rais Dkt Jakaya Kiwete akisalimiana na Mwambata mpya wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Kanali Adolph Mutta ambaye anachukua nafasi ya Brigedia Jenarali Emamanuel Maganga ambaye amemaliza muda wake.
 Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Afisa Ubalozi Emmanuel Swere kwenye hotel ya Ritz Calton wakati alipowasili Washington, DC.
 Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Afisa Ubalozi Catherine Kijuu.
 Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Mfanyakazi wa Ubalozi, Love Maganga.
 Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na mfanyakazi wa Ubalozi, Mayor Mlima.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na mfanyakazi wa Ubalozi Mariam Mkama.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na mfanyakazi wa Ubalozi Carol Mbilinyi.
 Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na mfanyakzi wa Ubalozi Rani Servin.
 Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na mfanyakazi wa Ubalozi, Eliud Mbowe.
Balozi wa Heshima kutoka San Francisco California, Ahmed Issa akisalimiana na Afisa Ubalozi Suleiman Saleh aliyesimama kati ni Sherry Julian (mke wa Ahmed Issa).
Picha ya pamoja.
[ Read More ]

BINTI WA NIGERIA ATANGAZWA KUWA MISS WORLD MUSLIMAH 2013

Binti wa kinigeria Obabiyi Aishah Ajibola mwenye umri wa miaka 21, jana ametangazwa kuwa mshindi wa shindano la Miss World Muslimah wa mwaka 2013 lililofanyika mjini Jakarta,Indonesia.

Mabinti 20 kutoka nchi sita ndio waliofanikiwa kuingia fainali ambapo washiriki wote walivaa hijabu na mavazi yaliyostiri maungo yao. Baada ya kuonesha watazamaji na wasomi wa kiislamu, jopo la majaji lilimchagua Obabiyi Aishah Ajibola kutoka Nigeria kuwa mshindi. Vigezo vilivyotumika kumpata mshindi ni Ufasaha wa kusoma Qurani na Maoni yao juu ya Uislamu katika Dunia ya kisasa.

Baada ya kusikia jina lake kama mshindi Obabiyi Aishah Ajibola, alilia kwa furaha na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yeye kuwa mshindi. “Jambo hili hasa si kushindana bali sisi tunajaribu tu kuonesha Dunia kwamba Uislamu ni mzuri” alisema Aishah.

Eka Shanti ambaye ndiye aliyeanzisha shindano hili miaka mitatu iliyopita, baada ya kupoteza kazi yake ya utangazaji wa Televisheni kwa kukataa kuvua Hijabu akiwa anatangaza, anasema, "Mwaka huu tumefanya makusudi lianze shindano letu kabla ya Miss World ili kuonesha kwamba kuna jambo mbadala na mfano wa kuigwa kwa wanawake wa kiislamu.”




Shindano hili lilianza mwaka 2011 likiwa na jina tofauti lilishirikisha waindonesia peke yake. Shanti anasema baada vyombo vya habari kulinganisha na Miss World tulibadilisha jina na tulikubali kuweka wagombea wa kigeni mwaka huu. Washiriki wa nje ya Indonesia, walitoka nchi za  Iran, Malaysia, Bangladesh, Brunei, na Nigeria.
Obabiyi Aishah Ajibola

Akivishwa Taji

Akivishwa beji ya Miss world Muslimah
Akishangilia kwa kushukuru baada ya kuangazwa mshindi

Washiriki wa Miss World Muslimah
[ Read More ]