Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

BINTI WA NIGERIA ATANGAZWA KUWA MISS WORLD MUSLIMAH 2013

-
Rehema Mwinyi.

Binti wa kinigeria Obabiyi Aishah Ajibola mwenye umri wa miaka 21, jana ametangazwa kuwa mshindi wa shindano la Miss World Muslimah wa mwaka 2013 lililofanyika mjini Jakarta,Indonesia.

Mabinti 20 kutoka nchi sita ndio waliofanikiwa kuingia fainali ambapo washiriki wote walivaa hijabu na mavazi yaliyostiri maungo yao. Baada ya kuonesha watazamaji na wasomi wa kiislamu, jopo la majaji lilimchagua Obabiyi Aishah Ajibola kutoka Nigeria kuwa mshindi. Vigezo vilivyotumika kumpata mshindi ni Ufasaha wa kusoma Qurani na Maoni yao juu ya Uislamu katika Dunia ya kisasa.

Baada ya kusikia jina lake kama mshindi Obabiyi Aishah Ajibola, alilia kwa furaha na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yeye kuwa mshindi. “Jambo hili hasa si kushindana bali sisi tunajaribu tu kuonesha Dunia kwamba Uislamu ni mzuri” alisema Aishah.

Eka Shanti ambaye ndiye aliyeanzisha shindano hili miaka mitatu iliyopita, baada ya kupoteza kazi yake ya utangazaji wa Televisheni kwa kukataa kuvua Hijabu akiwa anatangaza, anasema, "Mwaka huu tumefanya makusudi lianze shindano letu kabla ya Miss World ili kuonesha kwamba kuna jambo mbadala na mfano wa kuigwa kwa wanawake wa kiislamu.”




Shindano hili lilianza mwaka 2011 likiwa na jina tofauti lilishirikisha waindonesia peke yake. Shanti anasema baada vyombo vya habari kulinganisha na Miss World tulibadilisha jina na tulikubali kuweka wagombea wa kigeni mwaka huu. Washiriki wa nje ya Indonesia, walitoka nchi za  Iran, Malaysia, Bangladesh, Brunei, na Nigeria.
Obabiyi Aishah Ajibola

Akivishwa Taji

Akivishwa beji ya Miss world Muslimah
Akishangilia kwa kushukuru baada ya kuangazwa mshindi

Washiriki wa Miss World Muslimah

One Response so far.

  1. Mbunge says:

    Jamani haya si katika uislam, hata tujifanye eti tuna mashindano yetu ya umisi bado tunasahau kuwa mwanamke ana haya na kumuweka majukwaani eti kuwashindanisha umissi ni kinyume na uislam. Kwa mwendo huu utasikia kuna pombe za kiislam.

Leave a Reply