Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Profesa Mwandosya Ziarani India

mwa6.jpg (428×315)
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya yuko india wiki hii kwa ziara fupi kwa mwaliko wa Dr Rajendra Pachauri (pichani shoto) Mkurugenzi mkuu wa Tata Energy and Resource Institute (TERI) na Mwenyekiti wa Jopo la kimataifa la Wataalam wa mabadiliko ya Tabiachi (International Panel on climate Change IPCC) DrRajendra Pachauri ni mshindi wa tuzo ya Nobel ya Amani ya mwaka 2009 ambayo akiwakilisha IPCC alipokea tuzo pamoja na Bw. Al Gore Makamu wa Rais Msitaafu wa Marekani.Profesa Mwandosya na Dr Pachauri wamezungumzia maswala ya maji, nishati, mazingira, maliasili,ushiriano na maendeleo endelevu. Profesa Mwandosya ametembelea Chuo Kikuu cha TERI na Kituo Kikuu cha utafiti cha TERI.
mwa5.jpg (432×322)
Profesa Mwandosya akimkabidhi zawadi Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha TERI, Profesa Bhavit Bakishi.
mwa4.jpg (384×284)
Profesa na Mama Mwandosya wakipata maelezo ya utafiti katika matumizi ya mionzi ya jua kwa umeme wa nyumbani katika maabara ya chuo kikuu cha TERI
mwa3.jpg (382×283)
Profess akipata maelezo kuhusu biotechnologia katika kituo cha utafiti cha TERI nje kidogo ya new Delhi


mwa2.jpg (365×255)
Profesa Mwandosya alipata nafasi kuwatembelea wa Tanzania waliolazwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi. Hapa anasalimiana na Meja Generali (Msitaafu) Silas Mayunga
mwa1.jpg (478×312)
Profesa Mwandosya akiwa na badhi ya wafanyakazi wa ubalozi, new delhi, India. Toka shoto ni Mama Kiondo, Profesa, Nd. Mwamanenge na Mama Amina

[ Read More ]

TITANIC ACTRESS DIES AT 100

Veteran hollywood actress Gloria stuart.best remembered as the elderly kate winslet in oscar-winning superhit TITANIC dies on sunday night at her west los angeles home.she wa 100..
[ Read More ]

UZUSHI KUHUSU MADHARA YA MAWASILIANO YA SIMU





JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UZUSHI KUHUSU MADHARA YA MAWASILIANO YA SIMU

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepata malalamiko kutoka kwa watumiaji wa simu za mkononi kwamba kuna ujumbe unaosambazwa kwamba ukipokea simu utapata madhara.

Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujumla kwamba taarifa zinazoenezwa ni za uzushi na sio za kweli. Wananchi wanaombwa kupuuza uzushi huo kwa kua hauna ukweli wowote.
Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna tafiti nyingi zimefanyika sehemu nyingi duniani, ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. Mamlaka inashauri watumiaji wa huduma na wananchi wote kwa ujumla, kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya zikiwemo za mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta, ambazo hutumiwa ulimwenguni kote bila kuleta madhara yoyote.
Madhumuni ya Mamlaka ya Mawasiliano na watoa huduma za mawasiliano kwa ujumla ni kuwaletea wananchi wa Tanzania mawasiliano bora kwa kujenga miundombinu, kutoa huduma bora na matumizi mema.

Uzushi unaoenea upuuzwe kwa kuwa hauna ukweli wowote.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
03 Septemba 2010
[ Read More ]

Asha Ngedere: Ze Komedi

[ Read More ]

Orijino komedi na uchawi na wanga

[ Read More ]

WAZAZI WA MTOTO ALIYEZALIWA MZUNGU UINGEREZA KUPIMWA DNA



WAZAZI wa mtoto aliyezaliwa mzungu nchini Uingereza wamekubali uamuzi wa wataalamu wa vina saba kumfanyia uchunguzi mtoto huyo.

Habari kutoka nchini humo zimeeleza kuwa wazazi hao Benjamin na Angela wamekubali mtoto huyo wa kike afanyiwe uchunuzizaidi ili kuibaini sababu za kuzaliwa akiwa katika hali kama hiyo.

Mtaalamu wa vina saba kutoka Chuo Kikuu cha London Dkt.Mark Thomas amesema kuwa ana wasiwasi huwenda kuna mchanganyiko wa chembechembe nyeupe na zile na zile zinasobabbisha mtu kuwa na ulemavu wa ngozi albino.

Baba mzazi wa binti huyo Benjamni kwa upande wake amesema kuwa lichabya kukubali matokeo ya jinsi mtoto huyo alivyo,bado wataendelea kutafuta sababu za mtoto huyo kuzaliwa hivyo.

Mtoto huyo alizaliwa na wazazi weusi ambao ni raia wa Uingereza wenye asili ya Nigeria na inaelezwa kuwa katika familia yao hawana historia ya kuzaliwa mtu wa aina kama hiyo.Benjamin ambaye ni mshauri wa huduma kwa wateja alisema kuwa alipomuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza alishtuka lakini baadaye akasema kuwa ni mwanaye na anamuamini sana mkewe.

Alisema mkewe ni mwaminifu kwake sana na walihamia nchini humo wakitokea Nigeria miaka mitano iliyopita. 

[ Read More ]

BREKING NYUUUUZZZZZ: PROFESA MWAIKUSA AUWAWA JIJINI DAR


Marehemu Profesa
Jwani Timothy Mwaikusa

Habari zinasema Wakili na Mwanasheria nguli na Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es salaam Prof. Jwani Timothy Mwaikusa amefariki dunia baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati akirejea nyumbani kwake maeneo ya Salasala jijini Dar es salaam.

Prof. Mwaikusa pia alifanya kazi katika mahakama ya kimataifa ya I.C.T.R Arusha na alikua rafiki wa mahakama ambaye alitetea vizuri hoja alizowasilisha kuhusu mgombea binafsi.

Kwa wale waliosoma literature A- Level kama mimi, Prof. Mwaikusa pia alikua mwandishi mzuri wa poems ambazo wengi wetu tulizijibia mitihani.
Pamoja nae pia ameuwawa mwanae aliyekua akitoka nje kumfungulia geti, na mtu baki aliyekua akipita njia.

Kwa jicho la kawaida tu, haya yatakua mauaji ya kisasi au ya kumnyamazisha kuhusu jambo fulani kwakua habari za awali zinasema wauwaji hao hawakuiba kitu chochoteSee More

source:issa michuzi.
[ Read More ]

RAIS KIKWETE AMTEUA RASMI DR GHALIB BILAL KUWA MGOMBEA MWENZA



Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia chama cha Mapinduzi CCM rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dr. Ghalib Bilal kutoka Zanzibar kuwa mgombea mwenza kupitia CCM kwenye uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi ujao utakaofanyika Oktoba mwaka huu na kupelekea ukumbi mzima wa Chimwaga kulipukwa na mayowe ya vifijo na nderemo.
[ Read More ]

WASIFU WA DR MOHAMED ALI SHEIN


Dk. Ali Mohamed Shein alizaliwa Machi 13, 1948 katika Kijiji cha Chokocho kilichoko Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba. Dk Shein ameoa, ana watoto na wajukuu.
ELIMU
Msingi na sekondari
Alipata elimu yake ya msingi na sekondari kisiwani Unguja. Elimu ya msingi alisoma katika Shule ya Wavulana Gulioni kati ya mwaka 1956 na 1964 na alijiunga na Shule ya Sekondari Lumumba mwaka 1965 na kuhitimu mwaka 1968.
Elimu ya Juu
Mwaka 1969 alikwenda nchini Urusi na kujiunga na Chuo Kikuu cha Vorenezh (State University) kwa kozi ya maandalizi ya mwaka mmoja kabla ya kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu. Baada ya kuhitimu kozi hiyo (mwaka 1970) alijiunga na Chuo Kikuu cha Odessa kusomea masuala ya tiba ya magonjwa ya binadamu (medical biochemistry) hadi mwaka 1975 alipohitimu na kutunukiwa shahada ya uzamili. Alirudi nyumbani kufanya kazi hadi mwaka 1984 alipokwenda nchini Uingereza kuchukua masomo ya shahada ya juu ya Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Newcastle Upon Tyne. Alihitimu masomo hayo mwaka 1988 na kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika “Clinical Biochemistry and Matabolic Medicine” akiwa amejikita katika eneo kwa jina la kitabibu “Inborn errors of Metabolism”.
MAFUNZO MENGINE
Mbali na mafunzo hayo, Dk. Shein alipata mafunzo mengine mbalimbali katika fani ya tiba na uongozi ndani na nje ya nchi. Miongoni mwayo ni mafunzo juu ya utiaji na utoaji damu pamoja na namna ya uendeshaji wa Benki za Damu (Blood Transfusion Services and Operation of Blood Banks) yaliyofanyika mwaka 1981 Stockholm, Sweden. Mafunzo ya Menejimenti na Uongozi (A course in Management and Situation Leadership) yaliyofanyika Dar es Salaam, mwaka 1994 na Mipango kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi Katika Nchi Zinazoendelea (Planning for HIV/AIDS in Developing Countries) yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha East Anglia, Norwich nchini Uingereza mwaka 1995.
UZOEFU WA KITAALUMA
Mara baada ya kuhitimu elimu ya sekondari, Dk. Shein aliajiriwa kama karani katika Wizara ya Elimu, Zanzibar Mei, 1969 na baada ya muda aliongezewa majukumu ya kuwa Msaidizi wa Katibu Mkuu ‘B’ katika wizara hiyo; majukumu aliyoyatekeleza kwa pamoja hadi Septemba, 1969 ambako aliondoka kwenda masomoni nchini Urusi.
Baada ya kurejea aliteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Huduma za Maabara katika Wizara ya Afya, Zanzibar mwaka 1979 na kudumu katika nafasi hiyo hadi mwaka 1984 alipoondoka tena nchini kwenda nje kwa masomo ya Shahada ya Uzamivu. Alirejea nchini mwaka 1989 ambako aliteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Patholojia katika Wizara ya Afya, Zanzibar. Mwaka 1991 aliteuliwa kushika nafasi ya Meneja wa Mradi wa Kudhibiti Ukimwi, Zanzibar huku akiwa na majukumu mengine ya kutoa ushauri kwa Wizara hiyo katika masuala ya Huduma za uchunguzi wa magonjwa ya binaadamu na huduma za maabara (clinical biochemistry and Diagnostic Services).
UZOEFU WA UONGOZI NA SIASA
Dk Shein alianza kujishughulisha na masuala ya siasa tangu akiwa kijana mdogo wakati akiwa mwanafunzi. Alijiunga na Umoja wa Vijana wa chama cha Afro Shirazi tangu akiwa shuleni ambapo mwaka1968 aliteuliwa kuwa Katibu wa Habari wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Afro-Shirazi skuli ya sekondari ya Lumumba. Akiwa nchini Urusi alichaguliwa Rais wa Chama cha Wanafunzi wa Tanzania,Odessa mwaka 1973-1975. Dk Shein ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa Chama cha Mapinduzi kilichozaliwa mwaka 1977 kufuatia kuunganishwa vyama vya TANU na ASP. Amekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi tangu mwaka 1997 hadi sasa na amekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu tangu mwaka 2001 hadi sasa.
Dk Shein aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar tarehe 29 Oktoba 1995 na tarehe 13 Novemba aliapishwa kuwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar. Alishinda uchaguzi wa nafasi ya Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Mkanyageni, Kisiwani Pemba Novemba mwaka 2000 na kuteuliwa kushika nafasi mpya ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Katiba na Utawala Bora katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Alidumu katika wadhifa huo hadi tarehe 13 Julai 2001 alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha Makamu wa Rais aliyemtangulia Dk Omar Ali Juma kilichotokea 4 Julai 2001.
Alikuwa mgombea mwenza wa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi, alitangazwa tena na Tume ya Uchaguzi kuwa Makamu wa Rais tarehe 17 Disemba 2005 kufuatia ushindi wa Mgombea wa CCM Rais Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Aliapishwa kushika wadhifa huo tena tarehe 21 Disemba 2005 nafasi anayoendelea nayo hadi sasa.
MACHAPISHO NA UANACHAMA KATIKA VYAMA VYA KITAALUMA
Dk Shein ameandika na kuchapisha makala mbali mbali za kitaaluma ikiwemo zile za tafiti za shahada za uzamili na uzamivu.Ni mwanachama wa vyama vya kitaalumambalimbali na amekuwa akishiriki katika Mabaraza na Kamati mbalimbali kwa nafasi tofauti. Miongoni mwao ni kwa mfano alikuwa Mjumbe wa Association of Clinical Biochemists of the United Kingdom (1984-1989), Katibu wa Baraza la Utafiti la Wizara ya Afya Zanzibar (1989-1995). Mjumbe wa Kamati ya Taifa ya Ukimwi (1989-1995),Mjumbe wa Bodi ya Taaluma ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba Muhimbili (1990-1995),Mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Tekinolojia-COSTESH (1990-1995) na Mjumbe wa Chama cha Mapatholojia wa Nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika(1990-1995).


source:kwanza jamii.
[ Read More ]

BREAKING NEWS......


NI DR MOHAMMED SHEIN, amechaguliwa kuwa mgombea Urais Zanzibar. Amepata kura 117, Bilal 54, Nahodha 33

[ Read More ]