Mkazi wa Kijiji cha Hombolo, mkoani hapa, Chibenene Fwaru (50) aliyekuwa ametoka gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Omar Mganga alisema Polisi inaendelea na msako wa waliohusika katika tukio hilo lilitokea juzi kijijini hapo.
Kamanda alisema Chibenene alikatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake. Kwa mujibu wa Kamanda, awali mkazi huyo aliwahi kupigwa mshale mguuni na watu wasiojulikana.
Inadaiwa kuwa kijana huyo alikuwa akituhumiwa kwa mauaji ya watu wawili kijijini hapo lakini alitoka gerezani kwa msamaha wa Rais kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kiliwaudhi wananchi hao na kuamua kumuua kijana huyo. Kamanda Mganga alisema watu waliohusika kwa mauaji hayo, walikimbia. Alisema Polisi inawasaka kwa lengo la kuwafikisha mahakamani watakaobainika kuhusika.
Categories: