Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Nahodha meli iliyozama atahadharisha kuhusu uopoaji

-
Rehema Mwinyi.


NAHODHA wa meli ya MV Fatih iliyozama katika Bandari ya Malindi mjini Zanzibar wiki iliyopita, ameonya kuwa jitihada za kuopoa meli hiyo zisipofanywa kwa umakini, zinawesababisha uharibifu utakaosabaisha uchunguzi wa ajali hiyo kutokwenda sawa.

Akizungumza na Mwananchi jana ikiwa ni mara yake ya kwanza kuzungumza tangu kutokea kwa ajali hiyo, Nahodha Usi Ali Ussi, alisema taarifa kuwa meli hiyo inamomonyoka kutokana na kuchakaa wakati wa kuvutwa si za kweli.

Alisema tatizo ni watu kutofunga minyororo, katika sehemu ngumu za meli zilizowekwa maalum kwa kazi hiyo.

“Ikiharibiwa zaidi itasababisha uchunguzi uwe mgumu kwani chanzo cha ajali hiyo kitakuwa kigumu kugundulika…kinachotakiwa ni kujua kitu kilichosababisha meli kuzama ghafla” alisema.

Alisema wao wako tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka zinazohusika ili kuharakisha kazi ya kuopoa meli hiyo.

Nahoodha huyo ambaye ni Luteni kanali mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, pia alikanusha madai kuwa alipata matatizo kabla ya kutia nanga katika bandari hiyo, baada ya kukosa ushirikiano na watu wa bandari.

Alisema aliweza kuifikisha meli hiyo katika Bandari ya Malindi ikiwa salama na kufunga kamba gatini.

“Kama kungekuwa na tatizo muda mrefu ningeweza kuamuru wafanyakazi wawaandae abiria kwa tahadhari kwa kuwapa Life jackets, lakini tatizo lilitokea baada yakufika salama na baadhi ya abiria walikuwa wakiteremka.

Hata hivyo nahodha huyo alilalamikia kukosekana kwa taa katika bandari hiyo ambako kulisababisha juhudi za uokoaji kukwama.

Kwa mujibu wa nahodha huyo, wakati meli ilipoanza kulalia upande wa kushoto alikuwa katika chumba cha kuongozea meli na Mhandisi wa meli hiyo.

Alisema pia walikuwa na Afisa Mkuu wa meli na kwamba ghafla waliona chombo hicho kikiinama kwa kasi kubwa.

“Mimi niliruka kwenye mizigo nikatembea hadi nilipofika mwisho wa meli nikaruka katika kuta za gati ili kujiokoa.Kama tungejua kuwa hatari inayokuja tusingeliacha mizigo ndani ya vyumba na mpaka sasa vifaa vyetu bado havijatolewa.

Nahodha huyo ambaye aliendesha meli hiyo kwa takribani mwezi mmoja tangu ajiunge na kampuni hiyo, alisema hii ni ajali yake ya kwanza lakini amekuwa akipata matatizo madogo madogo tangu mwaka 1972 alipoanza kazi katika vyombo vya maji vinavyomilikiwa na jeshi.

Leave a Reply