Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Amuua mwenziwe kwa kumchoma kisu.

-
Rehema Mwinyi.


mwanafunzi mmoja wa darasa la sita anayejulikana kwa jina la Isaya Magese, 14, ameuawa kwa kuchomwa kisu na mwanafunzi mwenzake katika sehemu ya titi lake la kushoto
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Charles Nyanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 16 mwaka huu majira ya saa 1:00 jioni katika Kijiji cha Kisesa kilicho katika Kata ya Kolandoto, Shinyanga.


Alisema aliyefanya mauaji hayo, jina tunalihifadhi kwa sababu za kimaadili, ni mtoto wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sabamtaja aliyefanya mauaji hayo kuwa ni Shija Ndohoi (16) ambaye pia ni mwanafunziwa darasa la saba. Wote ni wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kisesa.

Kamanda Nyanda alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni ushabiki wa mpira ulioambatana na kurushiana maneno, huku Isaya akidaiwa kumwambia mwenzake kuwa anavuta bangi na kumuudhi mpinzani wake.

Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na linajiandaa kumpandisha kizimbani.


Leave a Reply