Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Mjukuu ambaka bibi yake, amuua

-
Rehema Mwinyi.


   KIJANA mmoja mwenye umri wa miaka 27 anatuhumiwa kumbaka kikongwe wa miaka 70, ambaye anasadikiwa kuwa ni bibi yake, na baadaye kumuua kwa kumchinja.

Kikongwe huyo, Kulwa Mahona, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mwagala, Kata ya Ibadakuli, aligundulika kufanyiw aunyama huo Mei 19 majira ya asubuhi.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Leonard Mayunga James aliiambiwa Mwananchi kuwa kijana huyo, ambaye jina tunalihifadhi, alimuua kikongwe huyo usiku wa manane baada ya kumuingilia nyumbani kwake alikokuwa amelala.
Alisema kijana huyo alianza unyama huo kwa kumbaka kwa nguvu na baadaye kumchinja shingoni baada ya kugundua kuwa kikongwe huyo alimgundua mbakaji.

Kijana huyo alitoroka baada ya akiamini kuwa ameshamuua kikongwe huyo, lakini kaka wa kijana huyo alipofika eneo hilo majira ya asubuhi alimkuta mzee huyo akiwa taaban kutokana na majeraha yaliyokuwa shingoni kwake na akawaita majirani.

Mwenyekiti huyo wa kijiji alisema kikongwe huyo alimudu kusimulia wanakijiji waliowahi kufika eneo hilo jinsi aliyofanyiwa ukatili na kijana huyo kutokana na ukweli kwamba wakati huo alikuwa akimudu kuongea.
Alisema waliamua kuripoti polisi na kuchukua fomu kwa ajili ya matibabu, lakini ilipotimia saa 9:00 alasiri kikongwe huyo alifariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Shinyanga.

Mtoto wa marehemu, John Njige alisema kuwa alipata taarifa za tukio hilo juzi asubuhi na kumkuta mama yake akiwa hospitalini na kwamba alipata nafasi ya kuzungumza nae kabla hajafariki dunia.
Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Isaya Nganga alisema alikuwa hajapata taarifa kamili za tukio hilo.

Leave a Reply