Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Komandoo Salmin Amour:Kwanini Ametua Dodoma?

-
Rehema Mwinyi.



RAIS wa Awamu ya Tano ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Salmin Amour Juma (mbele) akisalimiana na wakazi wa Dodoma waliofika kumpokea yeye na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha (nyuma) juzi.
--
Inasemwa, kuwa yapata miaka mitano sasa Komandoo Dr Salmin Amour, Rais Mstaafu wa Serikali ya Zanzibar hajapata kuhudhuria vikao vya chama chake, CCM. Kwamba Salmin Amour ameruka na kutua Dodoma inaonyesha jinsi mapambano ya kumpata Rais wa Zanzibar yalivyo magumu. Katika siasa, kwa komandoo kuruka na kutua Dodoma kuna tafsiri pia ya kuruka na kutua mahali pengine kabla ili kuweka mambo sawa. Ni wapi aliruka na kutua kimkakati kabla ya kutua Dodoma? Muda utakuja kutueleza. Lakini, picha ya hapo juu inatoa tafsiri nyingine kadhaa; je, ni bahati mbaya kwa Komandoo kupanda ndege moja na Shamsa Vuai Nahodha? Katika siasa muhimu ni timing ya tukio. Muda nao utatueleza.
Kwenye mnyukano unaoendelea sasa kule Dodoma kuna atakayehitaji ushiriki wa moja kwa moja wa komandoo Salmin ili aokolewe kisiasa. Na kazi hiyo Komandoo Salmin ana uzoefu nayo. Si wengi wenye kufahamu, kuwa ni Komandoo Salmin Amour aliyemwokoa John Malecela kwenye mdomo wa Nyerere pale Mwalimu alipokwenda Dodoma, kuwaita na kuwaambia ‘live’ Malecela na Kolimba kwamba muda wa kufungasha virago vyao umewadia, wajiuzulu, waondoke. Malecela alikuwa Waziri Mkuu katika utawala wa Mzee Mwinyi na Kolimba alikuwa Katibu Mkuu wa CCM. Itakumbukwa wakati huo kulikuwa na hoja ya kuundwa kwa Serikali tatu iliyokuwa ikichagizwa na Group of 55 likiwa na akina Njelu Kassaka, Philip Marmo na wengineo.
Wakati Kolimba alishamwambia mkewe na wanawe waanze kufungasha virago, Malecela alimtafuta Komandoo Salmin Amour na kumdokeza kilichotokea katika kuitwa kwao na Mwalimu. Ndipo hapo Salmin Amour akamwambia Malecela asubiri kwanza. Inasimuliwa, kuwa usiku huo kule Dodoma miaka ile ya tisini Komandoo Salmin aliwazungukia wajumbe muhimu wa CCM kutoka Zanzibar na kuwaweka sawa katika kumsaidia Malecela. Ukapatikana msimamo wa ‘ Kizanzibari’. Kilichotokea baada ya hapo inabaki kuwa historia.kwa Udani na Habari zaidi bofya na Endelea...>>>>>>>>>

Leave a Reply