Kifo cha Mtanzania mwenye asili ya Asia, Bw. Patel ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uhasibu na Ukaguzi wa Mahesabu ya P. S. Patel & Co, kilichotokea jana asubuhi baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya nne jengo la Red Cross jijini Dar es salaam, kimezua maswali mengi kuliko majibu. Kabla ya kutoka ofisini kwake na kwenda kujirusha, Patel aliacha ujumbe wa maandishi uliokutwa mezani kwake kuwa anaomba familia yake isiwabughudhi watoto wake. Hadi sasa haijulikani kitu kilichomuudhi Patel au kilichokuwa kero katika maisha yake mpaka kuamua kujiua. Pichani ni mwili wa marehemu Patel ukiwa sakafuni huku kichwa kikiwa kimepasuka na kulala kwenye dimbwi la damu. Picha hii ilipigwa na mpiga picha wetu muda mfupi baada ya kutokea tukio hili la kusikitisha.
..kabla ya kufika sakafu ya mwisho, Patel alijibamiza katika ngazi hizi za ghorofa ya kwanza (kwenye damu)
muonekano wa ngazi za ghorafa kuelekea juu alikopanda na kujitupa marehemu.
habari na global publishers