Mwanamuziki mkongwe nchini, Dk. Remmy Ongala amefariki dunia jijini Dar es Salaam leo.
Habari za awali zilizofikia mtandao huu zinasema Dk. Remmy alikata roho akiwa nyumbani kwake usiku saa nane na robo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kisukari.
Mwili wa marehemu umepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mipango ya mazishi bado haijajulikana.