MCHEZAJI wa Timu ya Usolo Abubakari Buba akijaribu kumpita mchezaji wa yimu ya Stone Town Juma Mbai katika mashindanoiya Kombe la Mapinduzi yanayafanyika uwanja wa Basketi Maisara timu ya Stone Town imeibuka na Ushindi.
WACHEZAJI wa Stone Town wakimsikiliza Mgeni Rasmin Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Hamad Masauni akitowa nasaha zake kwa wachezaji wa mchezo huo
WACHEZAJI wa timu ya Usolo wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mwenye suti Hamadi Masauni akizinduwa mashindano ya Kombe la Mapinduzi kutimiza miaka 47, uliofanyika kiwanja cha Maisara. <> MCHEZAJI wa timu ya Usolo Abubakari Buba mwenye mpira akimpita mchezaji wa timu ya Stone Town katika mchezo wa kuadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Maisara.
<>WACHEZAJI wa Timu ya Stone Town wakifahamishana jinsi ya kuwamiliki wapizani wao Timu ya Usolo katika mchezo wa maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi mchezo uliofanyika uwanja wa Basket Ball Maisara timu ya Stone Town imetoka na ushindi.