Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

BC EXCLUSIVE: MANGE KIMAMBI’s TELL-IT-ALL INTERVIEW - BongoCelebrity

-
Rehema Mwinyi.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa masuala ya watanzania mtandaoni,bila shaka utakubaliana nasi kwamba miongoni mwa mahali ambapo mengi hutokea na mengi huandikwa kama sio kujadiliwa basi mahali hapo ni katika blog inayokwenda kwa jina la U-turn.
Ni blog ambayo ingawa haina umri mkubwa(ilianzishwa mwaka mmoja na nusu tu uliopita), tayari imefanikiwa kuwa chanzo muhimu cha habari,michapo,maoni,matukio bila kusahau udaku wa hapa na pale.Ni mafanikio ambayo sio ya kubeza.It is what it is!
Mwendeshaji na mmiliki wa U-turn si mwingine bali Mange Kimambi ambaye miaka michache iliyopita ilikuwa ukisikia jina lake basi ilikuwa ni kupitia kurasa mbalimbali za magazeti hususani yale yanayoitwa “magazeti pendwa”. Leo hii mambo ni tofauti. Ni mama,mke,mwanafunzi na blogger mwenye idadi kubwa tu ya wasomaji na wafuatiliaji.
Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ya kina. Hii ni mara ya kwanza kwa Mange kufanya mahojiano ya kina na chombo chochote cha habari.
Je,Mange ni nani hasa?Ametokea wapi mpaka kufikia alipo hivi sasa ambapo kila siku idadi ya wasomaji na wanaofuatilia maisha yake na anachokiandika inazidi kuongezeka? Ni matukio gani katika maisha yake ambayo kwa namna moja au nyingine yamechangia in making her who she is today?
Nini siri ya mafanikio yake au ya blog yake?Unataka kujua ana maoni gani kuhusu mambo mbalimbali kama vile uongozi wa Rais Jakaya Kikwete?Ana ushauri gani kwa wasichana wadogo(teen girls)? Kwa majibu ya maswali hayo na mengine mengi,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;


BC: Mange,Karibu sana ndani ya BC.Mambo vipi?


MANGE: Asante sana.Feels good to be here!


BC:
Nimewahi kusoma mahali kwamba maisha yako ni kama vile kitabu kilicho wazi(an open book) ambapo kila anayetaka kusoma anayo nafasi ya kufanya hivyo.Lakini bila shaka utakubaliana nami kwamba wapo ambao hawajui lolote kuhusu historia ya maisha yako.Naomba tuanzie hapo…kwa kifupi tu ulizaliwa wapi,lini,ukasomea na kukulia wapi na mambo kama hayo.



MANGE: Nilizaliwa Hindu Mandal,Hospital- Dar es Salaam.Cheti changu cha kuzaliwa kina mwaka tofauti na passport yangu.According to my passport, I was born in 1980 lakini tukifuata Birth Certificate kuna difference ya 4years.Hii imetokana na kuna wakati mama yangu alitaka kunitoa kwa baba yangu akidai kwamba nina miaka chini ya 7.So kutokana na sheria za Tanzania natakiwa kuishi na mama. Baba yangu naye akawa na documents zake zinazosema nimeshapita miaka 7 kwa hiyo natakiwa kuishi na baba.So mama alikuwa na cheti changu cha kuzaliwa chenye umri tofauti na baba naye na passport yangu yenye umri tofauti.GO FIGURE.
Primary nilisoma Arusha School iliyoko Arusha- the best memories of my childhood came from my time there. Nilifanikiwa kufaulu mitihani ya darasa la 7 na nilichaguliwa kujiunga na Arusha Secondary.Baba yangu alifurahi sana na akanizawadia kwa kunipeleka kusoma Zimbambwe.So niliishi Harare miaka kadhaa kwa masomo yangu ya secondary.
Baada ya hapo nilikwenda Marekani kuanza masomo yangu ya juu.Kwa bahati nzuri (siwezi kusema bahati mbaya) nilijifungua mtoto wa kike,Bhoke, nikiwa Marekani jambo ambalo lilinifanya nirudi nyumbani kujipanga upya.
Then in 2004 nilijiunga na AVU-UDSM ambapo nilipata degree yangu ya Business Administration na sasa nipo Dubai nasoma Masters(MBA)
Mostly nimekulia Dar-es-salaam.


BC: Unakumbuka nini zaidi kuhusu maisha yako ya utotoni?Ulitaka kuwa nani,ulipenda michezo gani na tukio gani la utotoni ambalo hutokaa ulisahau?

MANGE: Yaani sijui pa kuanzia. Maisha yangu ya utotoni hayakuwa mazuri sana.,Mimi nimelelewa na baba yangu pamoja na mama yangu wa kambo. Baba alinipenda mno kama roho yake yote.Ila mama yangu wa kambo alinitesa sana.Niliishi maisha machungu sana enzi za utoto wangu. Huyu mama aliolewa na baba yangu nadhani kabla hata sijafikisha miaka miwili.Imagine mwanamke ukabidhiwe mtoto wa miaka miwili huyo mtoto si atadhani wewe ni mama yake?Ila mama yangu wa kambo alikuwa na roho mbaya sana.Alikuwa akinipiga sana,kunitukana sana,hanivalishi vizuri kama anavyowavalisha wanae.Alichokuwa akichukia zaidi ni mapenzi baba yangu aliyokuwa nayo kwangu. Ilifika stage nilikuwa nalilia kusoma boarding school ili tu niwe mbali naye.
Na kutokana na mateso niliyokuwa nayapata kwa mama yangu wa kambo, nilijikuta nimekuwa bully shuleni. Kwanza nilifukuzwa shule ya vidudu nikiwa na miaka 6 sababu ya kupiga watoto wa kihindi.Imagine miaka 6 nilifukuzwa shule!Primary nilisoma Arusha school, ambako huko ndo mpaka leo nina maadui sababu nilikuwa ni mwonevu sana.Nilikuwa napiga sana watoto wa wengine.Nilikuwa sisikii,nilikuwa mtoto mtukutu.
Baadaye nilikuja kuelewa kuwa hii yote ilitokana na mateso niliyokuwa napewa na mama yangu wa kambo nyumbani na ndio maana na mimi nilikuwa nikifika shule nawafanya watoto wengine kama mimi navyofanywa nyumbani kwetu.
Mama yangu wa kambo alikuwa ni mnyanyasaji sana wa wafanyakazi wa ndani. Nyumbani kwetu siku zote kulikuwa na vyakula vya aina mbili;chakula chetu cha familia na chakula cha wafanyakazi. Na wafanyakazi chakula chao ni ugali maharage au ugali na mchicha.Nyama wanakula mara moja kwa wiki,na wali pia wanakula mara moja kwa wiki.Ilikuwa inaniuma sana mpaka nikaanza tabia ya kupakua chakula kingiii ambacho siwezi kumaliza ili niwape angalau waonje.Yaani nilikuwa najiona na mimi nina hadhi kama ya wafanyakazi wetu kwa jinsi alivyokuwa akinichukia.Naamini angekuwa na uwezo hata mimi angekuwa akininyima chakula.
Leo hii ninavyoishi mimi,chakula ninachokula mimi ndicho anachokula mfanyakazi wangu.Hata siku moja sijawahi kumwambia ale tofauti na ninavyokula mimi.
Ila kwa upande mwingine yule mama kutokana na maisha magumu aliyonipa tangu nina miaka miwili mpaka nimekuwa mkubwa amenisaidia sana. Kutokana na yale mateso nilijifunza kuji-defend, nilijifunza kufight for myself na the biggest thing nilijifunza ni kwamba hata leo hii ningeolewa na mtoto mwenye mtoto asiye wa kwangu ningempenda huyo mtoto zaidi ya wa kwangu niliyemzaa.
KWA KWELI MY CHILDHOOD WAS THE WORSE PARTY OF MY LIFE,huwa sipendi hata kufikiria wala kukumbuka.Yule mwanamke aliniumiza sana,ila alisahau kwamba watu huwa wanakuja kuwa watu wazima na huwa hawasahau especially kama hujawahi hata kuomba msamaha kwa ulichofanya.
Kuhusu michezo;nilikuwa napenda michezo mingi sana. Nilipata bahati ya kwenda shule iliyokuwa inajali sana sports(Arusha School).Yani mimi ni nilikuwa kapteni wa michezo yote,swimming,kukimbia, na wakati na graduate nilipata tuzo ya sports girl of the year.
Tukio la utotoni ninalolikumbuka mpaka leo ni hili; nilisomaga Bunge Primary School kwa muda wa mwaka mmoja. Basi kuna wakati sikwenda shule kwa muda wa wiki 2 nilikuwa naenda kucheza. Baba yangu akapata taarifa siendi shule.Basi kesho yake akaenda na mimi mpaka shule, asubuhi wakati wa assembly akanichapa mbele ya shule nzima,yani viboko vya ukweli.Ilikuwa noma sana.


BC: Du,pole sana Mange. Kwa upande mwingine nilisikia kwamba wewe na mama yako wa kambo mnagombea mali za Marehemu Mzee Kimambi?Kuna ukweli katika hili?


MANGE: Sio ukweli, hatukuwa tukigombea.Ni kwamba tu baba yangu hakuacha will.So youu can imagine mtafaruko uliotokea hapo. Mimi niliridhia yeye awe msimamizi wa mirathi nikiamini kuwa atanipa kilicho changu.Ila nikaona muda unaenda sikabidhiwi share yangu ndio nikarudi mahakamani.
Anyways,mambo yanaenda vizuri tu sasa nimeshakabidhiwa mali kadhaa. Kabla ya mwisho wa mwaka tutakuwa tumeshamaliza makabidhiano.Shukrani nyingi zimwendee mwanasheria wangu Mama Tenga ambae alinipigania sana nipate share yangu na mpaka sasa bado ana fight on my behalf sababu mimi niko mbali.
Mange and her daughter,Bhoke.
BC: Nakumbuka Mzee kimambi alikuwa anamiliki Tiger Motel na lile jumba kubwa la kifahari Mbezi Beach,je bado unaishi pale unapokuwa Tanzania? Na ile hotel imeuzwa au la?


MANGE: Mimi na familia yangu nzima tumeishi kwenye ile nyumba Mbezi Beach tangu mwaka 1989 tulivyohamia kutoka Temeke. Nikiwa Dar siishi pale na sijaishi pale zaidi ya mwaka mmoja sasa kutokana na kutoelewana na matatizo ya hapa na pale.Ila kisheria ile nyumba ina milikiwa na watu wanne wakiwa ni mimi,wadogo zangu wawili na step mother wangu na nina haki ya kuishi pale muda wowote nitakaojisikia.Hata watoto wangu wana haki ya kuishi pale. Same na Tiger Motel wote tumeshamegewa share zetu mahakamani sasa nasubiri tu kukabidhiwa mshiko wangu sababu shareholders waliobaki wanataka kuni buy out ila kama ikishindikana mimi nita wa buy out au hotel itapigwa mnada kila mtu apewe chake.Ni hayo tu.
Naomba usiniulize swali lingine linalohusu mirathi ya baba yangu.It’s a very sensitive issue, especially ukizingatia kwamba huyo mama yangu wa kambo pia ndo mama wa kaka zangu wawili ambao nawapenda kupita kiasi.So tuachie hapa hii issue.


BC: Kama binadamu huwa tunapewa ushauri au mawazo mbalimbali.Ni jukumu na maamuzi yetu kuyazingatia au kuachana nayo.Kwa upande wako unaweza kukumbuka ushauri gani ambao unadhani ulikuwa wa maana zaidi na ambao umeuzingatia mpaka leo katika kuendesha maisha yako.Nani alikupa ushauri huo?


MANGE: Ushauri mzuri sana niliowahi kuupata katika maisha yangu ni kuhusu elimu.Baba yangu alikuwa mkali sana kwenye suala la shule.Siku zote alikuwa akiniambia bila shule sitokaa kuheshimwa. Pia Dr. Mwele Malecela amekuwa akinishauri kuhusu suala la shule mpaka leo hii. Na naweza kusema huu ushauri umenisaidia sana kwenye maisha yangu kwani nina uhakika chochote kikitokea kwenye maisha yangu elimu yangu itanistiri.
Na baada ya baba yangu kufariki ghafla na kutuacha tukiwa hatujui tuanzie wapi, nilijifunza kwamba mwanamke hutakiwi kujiweka tu bila shughuli yoyote au elimu sababu umeolewa na mtu mwenye uwezo kwani huwezi kujua Mungu kapanga nini.Kwa hiyo ni lazima kujidhatiti na elimu.ELIMU ITAKUSTIRI.


BC: Ni kitu gani kilichokushawishi kuanzisha blog ya U-Turn na kwanini jina U-Turn?Malengo yako ya awali yalikuwa ni yapi? Bado malengo ni yale yale au yamebadilika kidogo?


kusoma zaidi ingia humu.


http://www.bongocelebrity.com/2011/02/27/bc-exclusive-mange-kimambi%E2%80%99s-tell-it-all-interview/#more-10385

source:bongo celebrity

Leave a Reply