Hafla ya matokeo ya kusoma Qur'an ya mwaka 2010 (1431 AH) yamefanyika siku ya Alhamisi ya tarehe 03/02/2011 katika ukumbi wa Town Hall, East Ham, jijini London.
Washiriki wasiopungua 18 walishiriki mashindano hayo ya kusoma Qur'an yaliyoandaliwa na kituo cha kujitolea na kinachosaidia Waislamu waishio nchini Uingereza (Salama Trust).
Mashindano hayo yaligawanyuka katika makundi matatu. Mshindi wa kwanza katika kundi la kwanza alikuwa Khayrat Juma ambaye alipata kura 99%, mshindi wa pili katika kundi la kwanza alikuwa Yaaqub Abeid ambaye alipata kura 98% na mshindi wa tatu alipata kura 85%.
Kundi la pili, mshindi wa kwanza Rashid Mohammed alipata kura 100%, Mujahidi Mujahidi alitokea mshindi wa pili kwa kupata kura 94% na mshindi wa tatu Faisal Issa aliyepata kura 85%.
Ashraf Khalifa ndiye mshindi katika kundi la tatu kwa kupata kura 100%, Mohammed Yusuf alitokea mshindi wa pili kwa kupata kura 87% na Abdulmajid Yusuf alitokea mshindi wa tatu kwa kupata kura 64%.
Mwenyekiti wa Salama Trust Bw. Salehe Jaber aliwapongeza washiriki wote kwa kujitolea kushiriki mashindano hayo ya kusoma Qur'an.
"Umoja na ushirikiano ndiyo chanzo cha maendeleo" alisema Bw. Jaber na kusisitiza mshikamano kwa waislamu dunia kote.
Ally Muhdin - WWW.TZ-ONE.BLOGSPOT.COM