Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Taarifa Ya Habari Yasomwa Gizani Nepal

-
Rehema Mwinyi.


''Ifuatayo ni taarifa ya habari ikisomewa gizani, kwa kuwa umeme umekatwa.'' Mojawapo wa vituo vikuu vya televisheni nchini Nepal kimeanza kutangaza taarifa zake za habari za usiku katika mazingira ya nusu kiza ili kubainisha athari za ukataji mkubwa wa umeme.

Tangu mwanzoni mwa mwezi wa February, kituo cha televisheni cha Kantipur kimetumia taaa zinazotumia mafuta kutoa mwanga wakati wa taarifa yake ya habari ya dakika 30 saa moja usiku.

Mkuu wa kituo hicho alisema shabaha ni kutia shinikizo kwa serikali ikabiliane na tatizo hili.

Kwa sasa Nepal inakabiliwa na mpango wa kukata umeme kwa saa 12 kila siku.

"tunaitaka serikali izalishe umeme zaidi kwa haraka" mkuu wa Kantipur News Tirtha Koirala aliiambia BBC.

"hadi sasa watazamji wetu wamepokea vizuri hatua hii;lakini serikali bado haijasema chochote."

Licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme kutokana na mito, Nepal huzalisha nusu tu ya mahitaji yake ya umeme.

Miaka kumi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya waasi wa Kimao na serikali ya Nepal vilivyomalizika mnamo mwaka 2006, imemaanisha uwekezaji mdogo sana katika sekta ya umeme ya Nepal.

Juu ya yote hayo mtandao wa kusambaza umeme nchini uliathiriwa vibaya sana baada ya kuharibiwa na mafuriko ya mto Kosi mnamo mwaka 2008.

Hii imesababisha kuwepo na mgawo wa umeme kuwa ni jambo la kawaida katika maisha ya kila siku.

Tatizo ni kubwa zaidi katika majira ya baridi ambapo ukosefu wa mvua na kina cha chini cha mito inamaanisha mabwawa yaliyopo hayawezi kuendesha shughuli zao kikamilifu.

Mamlaka ya nguvu za umeme ya Nepal yanayomilikiwa na serikali yamesema kuwa nchi inaweza kutazamia kukatwa umeme kwa kipindi cha saa 14 kila siku katika muda wa wiki chache zijazo.

"tunasumbuka sana kwa sababu ya mgawo wa umeme ," amesema Bwana Koirala .

"Takriban wanafunzi 400,000 hivi sasa wanajitayarisha kwa mtihani wa shule za sekondari na hawana mwanga wowote wa taa usiku".

"Halikadhalika wafanyibiashara wadogo wadogo ambao hawawezi kumudu jenereta au kifaa cha "inverter"nao pia hawawezi kuendesha shughuli zao."

Bwana Koirala alisema taarifa za habari za kituo chake zitaendelea kutangazwa katika mazingira ya kiza mpaka serikali itakapochukua hatua .

Leave a Reply