Aliyekuwa rais wa Afghanistan Burhanuddin Rabbani ameuliwa baada ya mtu aliyelificha bomu kwenye kilemba chake kulilipua bomu hilo wakati wakisalimiana.
Rais Burhanuddin Rabbani ambaye pia alikuwa ndiye mkuu wa baraza kuu la kutafuta amani nchini Afghanistan, alifariki dunia baada ya mtu aliyekuwa akimuamini kumgeuka na kujilipua kwa bomu alilolificha kwenye kilemba chake. Wasaidizi wanne wa Rabbani nao walifariki dunia baada ya bomu hilo kulipuka wakati Rabanni aliposimama kumsalimia kwa kumkumbatia mwakilishi wa Talibani baada ya kumalizika kwa mazungumzo marefu baina yao ya kutafuta suluhisho la amani nchini Afghanistan. Fazel Karim Aymaq ambaye ni mjumbe wa baraza la amani la Afghanistan alisema kuwa watu wawili wanaoaminika sana walifika nyumbani kwa Rabbani mjini Kabul ili kuleta ujumbe wa amani toka kwa Talibani. "Mmoja wao alisalimiana na Rabbani kwa kuweka kichwa chake kwenye mabega ya Rabbani na kulilipua bomu alilokuwa amelificha kwenye kilemba chake", alisema Aymaq. Taarifa zaidi zilisema kuwa mjumbe huyo wa Talibani alikuwa akijulikana kama Mohammad Masoom na alikuwa akifahamiana vizuri sana na Rabbani akiaminika kuwa anatafuta suluhisho la amani. Masoom aliluwa akienda mara kwa mara nyumbani kwa Rabbani na aliwahi kumkaribisha Rabbani nyumbani kwake na alimpa ulinzi wa kutosha hali iliyomjengea uaminifu wa kutosha kwa rais huyo wa zamani. Masoom aliteuliwa na Talibani kuwa mwakilishi wa Talibani katika mazungumzo ya kutafuta suluhisho la amani kati ya Talibani na serikali ya Afghanistan. Kuuliwa kwa Rabbani ni pigo kubwa sana kwa rais wa Afghanistan, Hamid Karzai ambaye aliamua kukatisha ziara yake nchini Marekani na kurudi Afghanistan. Mamia ya watu waliandamana leo kwenye mitaa ya mjini Kage.bul kulaani kuuliwa kwa rais huyo mstaafu aliyekuwa akiheshimika kwa jitihada zake za kuleta amani kwenye nchi hiyo ambayo imeharibiwa kwa vita. "Alitaka amani nchini Afghanistan na alijitolea maisha yake kupigania njia ya kuleta amani", alisema mmoja wa waandamanaji hao. source nifahamis | ||