Katika tukio ambalo si la kawaida, hausigeli mmoja wa nchini Marekani ambaye alikuwa ni mnene sana, alizimia ghafla na kumuangukia mtoto mchanga wa mwezi mmoja na kupelekea kufariki kwa mtoto huyo kutokana na kuelemewa na uzito.
i na ni
Baba wa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Michael Baldwin II ambaye ni mwandishi wa habari jijini New York, alikuwa nyumbani kwake akimuangalia mtoto wake mchanga wa mwezi mmoja kabla kutakiwa aende kazini mara moja na mwajiri wake. Michael alilazimika kumuita hausigeli Teresa Coffey, ambaye pia alikuwa ni rafiki wa mke wake ili aje amtunzie mwanae huyo wa kiume. Alipofika kazini, Michael alijaribu kumpigia simu Teresa mara kadhaa ili kujua hali ya mtoto wake. Baada ya kuona simu haipokelewi, Michael alirudi nyumbani ili ajue nini kimetokea mpaka hausigeli hapokei simu. Michael alimkuta Teresa akiwa amefariki amelalia uso chini kwenye kochi huku akiwa amepiga magoti sakafuni. Michael hakumuona mwanae, alijaribu kuzunguka kila chumba kumtafuta mwanae lakini hakufanikiwa kumuona. Hisia zilimtuma amnyanyue Teresa na ndipo alipomkuta mwanae akiwa amefunikwa na uzito wa Teresa akiwa tayari ameishafariki. "Nilimnyanyua Teresa na kumkuta mwanangu chini yake, alikuwa amelala huku mikono yake akiwa ameiweka tumboni mwake", alisema Michael. "Alikuwa amebadilika rangi kuwa kama wa bluu, nilimnyanyua na kumuita jina lake , nilijua tayari mwanangu ameishafariki", aliongeza Michael. Taarifa ya polisi ilisema kuwa Teresa alikuwa ni mnene sana na alikuwa na matiti makubwa sana huenda nyama nyama za mwili wake zilimfunika mtoto na kumfanya akose pumzi. Taarifa zaidi zilisema kuwa Teresa alikuwa akijulikana kuwa alikuwa akisumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya na chupa ya dawa alizokuwa akizitumia ilikutwa pembeni yake. habari na nifahamishe. | ||