Familia ya Bw. na Bibi Edwin Dosantos wakazi wa Kimara jijini Dar es Salaam wanaomba msaada wa maziwa au fedha kwa ajili ya kuwasaidia kuwatunza watoto wao mapacha watatu ambao wana Umri wa miezi miwili.
Akizungumza na MO BLOG jijini Dar es Salaam Baba wa watoto hao Bw. Dosantos amesema kwa sasa yeye na mkewe hawana kazi na inawawia vigumu kutimiza mahitaji ya watoto hasa lishe kutokana na kwamba mama mzazi wa watoto hao hana maziwa ya kutosha kuwakidhi watoto hao.
MO BLOG inaomba kuwashirikisha wadau ambao wataguswa na malaika hawa kuwasaidia chochote kupitia namba ya mzazi wa kiume wa watoto hao au kwa kuwasiliana au kuwasilisha mchango wowote hasa maziwa.
Tunaamini kutoa ni moyo na si utajiri.