MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda, imemhukumu Haruna Ndayage (54), mkazi wa mtaa wa Kashaulili, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuingilia mkewe kinyume na maumbile.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi, Desdel Magezi, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.
Alisema shahidi wa tano ambaye ni daktari aliithibitishia mahakama kuwa mlalamikaji baada ya kufanyiwa uchunguzi iligundulika kuwa aliingiliwa kinyume na maumbile yake.
Aidha, alisema ushahidi uliotolewa na watoto wao ulionyesha kuwa Haruna alimfayia kitendo hicho mkewe, kwani watoto wote walimtaja baba yao ndiye mhusika wa kitendo hicho.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mshtakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu, kwani wakati akifanya kosa hilo hakuwa na akili timamu.
Alidai kwa miaka 24 waliyoishi na mkewe hakuwa na ugomvi wowote naye isipokuwa miezi sita kabla ya tukio hili waalikuwa na ugomvi ugomvi ambao hakuweza kuueleza mahakamani hapo.
Hata hivyo, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Finias Mjula, alipinga utetezi huo na kuiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili awe mfano kwa watu wengine wenye tabia ya kuwadhalilisha wake zao.
Awali katika kesi hiyo, ilidaiwa kuwa Oktoba 28, mwaka jana, majira ya saa 12 alfajiri, mshtakiwa alimwingilia kinyume cha maumbile mkewe.
Kumuingilia mkewe kule kulikokataziwa ni makosa.
Kifungo kesha pewa,jee baada ya kumaliza kifungo chake
ataweza kumrejea mkewe - au talaka ameshatowa kisheria?
Naamini hivyo ndivyo itavyostahiki.Mzee huyu pengine naye
atakomeshwa na wenziwe huko jela,aliwe kiuwa na yeye akome .