Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Bi Tele na Wasanii Wezake Chupuchupu Kupata Kipigo

-
Rehema Mwinyi.


Wasanii wa maigizo wa kikundi cha Valentine Arts Group cha mtaa wa Jang'ombe, juzi walinusurika kupata kipigo baada ya watu waliohudhuria onesho lao kuzusha vurugu, na wasanii hao kuokolewa na polisi.
Onesho la kikundi hicho lilifanyika katika skuli ya Chumbuni kwa kutunia umeme wa jenereta kutokana na juzi Jumapili nishati hiyo kuzimwa nchi nzima kwa ajili ya matengenezo katika kituo cha Ubungo mjini Dar es Salaam.
Vurugu hizo zilianza mara baada ya kuharibika kwa jenereta hali iliyosababisha kuvunjika kwa onesho hilo.

Hali hiyo iliwafanya baadhi ya watu waliohudhuria kuanza kurusha mawe dhidi ya wasanii hao akiwemo mwanamama aliyejipatia umaarufu kwa jina la Bi Tele anayeigiza uchawi katika igizo la ‘Husdaa’ linalorushwa kila siku ya Jumatano katika kituo cha ZBC Televisheni.
Akizungumza na gazeti hili mara baada ya polisi kudhibiti ghasia hizo, Mwalimu msaidizi wa kikundi hicho Samuel Said Makunga, alisema vitendo hivyo si uungwana, na kwamba wananchi hao hawakupaswa kufanya fujo na badala yake walikuwa wasubiri.
Naye msanii anayetikisha katika igizo la ‘Husdaa’ Bi Tele, alilaani vitendo hivyo na kuongeza kuwa akili za vijana waliohusika navyo zinasumbuliwa na bangi.
Kwa upande wao, baadhi ya wapenzi wa sanaa waliokuwepo, walidai kuwa walilazimika kufanya hivyo kwani tayari walikwishalipa fedha ili kupata burudani hiyo, na kwamba waliamua kuwapa fundisho wasanii hao.

Leave a Reply