MKAAZI wa Kwaalimsha, Habiba Juma Ramadhani (42) amefariki dunia baada chumba alichokuwa amelala kuteketea kwa moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohammed alisema moto huo uliotokea juzi majira ya saa 2:00 pia ulimjeruhi Hassan Shaabani Idd (48), ambaye alilala katika chumba hicho.
Alisema kabla ya chumba walicholala marehemu na majeruhi huyo kuteketea kwa moto walikuwa wamewasha mshumaa ambapo ulipokaribia kumalizika ulirukia vitu vyengine chumbani na kuripuka.
Kamanda huyo alibainisha kuwa ilikuwa vigumu kujiokoa kwani inasemekana walilewa kabla ya kuchukuliwa na usingizi.
Kamanda Azizi alifahamisha kuwa, sambamba na matukio hayo vitu vilivyokuwemo ndani humo viliteketea kwa moto na hadi hivi sasa hakuna idadi kamili ya hasara iliyopatikana.
Baada ya majira ya saa 4 hadi 5 usiku watu walishitukia moto umeshika kasi katika chumba hicho cha bandani na wakiwa bado wamelala.
Katika kufanikisha tukio hilo jitihada za watu na kikosi cha Zimamoto na Uokozi zilifanyika kuokoa jitihada za zimamoto ndipo ziliwasaidia kuokoa majeruhi hao.
Lakini jitihada hizo zilipoendelea baada kupatikana mwanamke huyo ameshaungua vibaya sana na kupatikana amefariki muda mfupi na kufikishwa hospitali ya mnazi mmoja na kufanyiwa uchunguzi.
Katika chumba hicho vimeungua vitu vyote na katika nyumba hiyo chumba hicho pekee kilicho teketea kila kitu.
Categories: