Amesema kamwe hakufanya hivyo, pamoja na kwamba walikuwa wamekwaruzana kwa muda mfupi na akaenda kuoga, akiwa anatoka bafuni alianguka (aliteleza) na kugonga kichwa kabla ya kukutwa na umauti.
Binti huyo ameiambia Polisi kwamba Kanumba (ambaye wamekuwa na uhusiano naye wa mapenzi kwa muda sasa) alikuwa 'amebugia' ujazo mkubwa wa pombe kali aina ya Jackie Daniels (JD).
TAJOA itaendelea kuujuza umma juu ya kila kinachoendelea juu ya mkasa huu unaoonekana kuvuta hisia za Watanzania wengi na hata wale walio nje ya nchi.
chanzo TAJOA.