Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

RAIS DK. SHEIN AZINDUA BOHARI KUU YA DAWA ZANZIBAR

-
Rehema Mwinyi.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi
wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa,Maruhubi Nje ya Mji wa Zanzibar jana
ikiwa ni shamra shamra za kilele  cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu
ya zanzibar,(kulia)  Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso
Lenhardt.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kama ishara ya uzinduzi
wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa,huko Maruhubi Nje ya Mji wa Zanzibar
jana ikiwa ni shamra shamra za kilele  cha miaka 49 ya Mapinduzi
Matukufu ya zanzibar,(kulia) ni Naibu waziri wa Afya Sira Ubwa Mamboya
na  Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhardt.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa
Bohari Kuu,Said Mohamed,(kulia) alipotembela sehemu ya kuhifadhia
Dawa,baada ua uzinduzi wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa huko Maruhubi
Nje ya Mji wa Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za kilele  cha miaka 49
ya Mapinduzi Matukufu ya zanzibar,(wa tatu kushoto)  Balozi wa
Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhardt.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu Kulia)pamoja na Viongozi
wengine akiwemo Balozi wa Marekani Nchini  Alfonso
Lenhardt.wakiangalia namna ya uchukuwaji dawa kwa kutumia mashine
maalum na kutoa nje ya Bohari kuu ya Dawa,baada ya ufunguzi rasmi jana
huko Maruhubi Nje ya mji wa Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za kilele
cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzíbar  
………………………………………………
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema uzinduzi wa Bohari kuu ya Dawa utaiwezesha Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar kupanga bajeti yake vyema ya dawa na kusaidia utoaji wa huduma za afya kwa ubora wa hali ya juu.
 Rais Shein ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Bohari Kuu ya Dawa iliyopo Maruhubi mjini Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Amesema Bohari hiyo ya kisasa ni matunda ya kujivunia ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kwa hakika italeta tija katika upatikanaji wa dawa na uimarisha wa afya za wananchi.
 Dkt. Shein ameelezea matumaini yake kwa sekta ya afya kupitia Bohari hiyo na kwamba anaamini baada ya miaka mitatu Zanzibar itakuwa haipeleki tena Wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
 Aidha Dkt. Shein amewataka watumishi wa Serikali kubadilika kiutendaji kulingana na kasi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa Bohari hiyo kuitunza vyema ili iendelee kutoa huduma kama inavyotakiwa.
 Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Sira Ubwa amesema Bohari hiyo itaboresha utoaji wa huduma kwa uhakika kutokana na ubora wa vifaa na mitambo ya kisasa ambapo wataalamu wataweza kubaini mahitaji ya Dawa zinazohitajika katika kila Hospitali za Unguja na Pemba.
 Kwa upende wao Mabalozi wa Marekani na Denmark wameelezea kufurahishwa kwao na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha afya ya Wananchi hasa katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria na Ukimwi.
 Aidha wameahidi kuendelea kutoa mashirikiano kwa Serikali hasa katika huduma za Afya kwa Mama na Watoto, Elimu,Mapambano dhidi ya magonjwa ya maambukizi pamoja na uzazi wa mpango.
 Bohari hiyo iliyojengwa na Serikali ya Mapinduzi kwa msaada wa Shirika la USAID na NIDA inaelezewa kuwa ya tatu duniani katika viwango vya ubora ambapo jumla ya Dolla za Kimarekani Milion 1.2 zimetumika kukamilisha ujenzi wake.

Leave a Reply