Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Bi Kidude Wakati wa Uhai wake

-
Rehema Mwinyi.



BiKidude akiwa katika viwanja vya Ngome Kongwe wakati wa Tamasha la Sauti za Busara 
 BiKidude akipinga ngoma aina ya Uyango katika matamasha yanayofanyika Zanzibar katika viwanja vya Ngomekongwe
 Mwaka 2005 huko Gateshead, Newcastle nchini Uingereza,Bi.Kidude alipokea tuzo yenye heshima kutoka World Music Expo (WOMEX) kwa mchango wake katika muziki na utamaduni wa Zanzibar. Katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda wanamuziki mahiri kama Peter Gabriel, Miriam Makeba na wengineo. Bi.Kidude anasema hawezi kuacha kuimba mpaka siku atakapoiaga dunia kwani akiimba anajihisi kuwa binti wa miaka 14!


Mwaka jana, kampuni ya nchini Uingereza iitwayo ScreenStation kwa kushirikiana na Busara Promotions walitoa documentary iitwayo “As Old As My Tongue-The Myth and Life of Bi.Kidude” inayoelezea historia nzima ya maisha yake. Unaweza kuona dakika kama saba hivi za documentary hiyo hapa chini.Anasema yeye anakunywa na pia anavuta,lakini zaidi ya yote anaweza kuimba bila hata kutumia spika ya mdomo yaani microphone.
Picha hii ni kwa hisani ya Marcel Mutsaers aliyompiga Bi.Kidude wakati wa Tamasha lijulikanalo kama Festival Mundial kule Tilburg-Uholanzi mwezi June mwaka 2006.


Umri wake halisi haujulikani. Kinachojulikana ni kwamba ana umri zaidi ya miaka 90 na hivi sasa sio ajabu akawa ameshafikisha umri wa miaka 100! Amekuwa muimbaji tangu miaka ya 1920 akiwa ni mfuasi wa Sitti Bin Saad mmojawapo wa waimbaji wa mwanzo kabisa wa taarabu visiwani Zanzibar.

Hivi leo anatambulika na kuheshimika kama malikia wa taarabu na mambo ya unyago asiye na mpinzani. Alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo katika familia ya watoto saba. Jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa ni Fatuma Binti Baraka kabla jina maarufu la Bi.Kidude halijashika baadaye alipoanza kuwa maarufu katika uimbaji.Wazazi wake walikuwa ni wafanyabiashara ya kuuza nazi enzi hizo za Zanzibar iliyokuwa chini ya utawala wa wakoloni.

Katika mahojiano mbalimbali aliyofanya na vyombo tofauti tofauti vya habari ulimwenguni Bi.Kidude anasema alianza kuimba akiwa na umri mdogo wa miaka 10. Anasema uimbaji alijifunza kutoka kwa Sitti binti Saad tena kwa kujificha nje ya nyumba na kumsikiliza Sitti binti Saad akiwaimbia wageni ambao mara nyingi walikuwa wakipelekwa pale na yeye Bi.Kidude.

Akiwa na umri wa miaka 13 tu hakuwa na jinsi bali kukimbilia Tanzania bara(Tanganyika enzi hizo) ili kuepuka kuozeshwa kwa nguvu. Akiwa Tanzania bara alizunguka kila kona ya nchi akiwa muimbaji katika makundi mbalimbali ya muziki wa taarabu likiwemo lile maarufu la Egyptian Musical Taarab. Baadaye alihamia nchini Misri kwa kifupi kabla hajarejea kisiwani Zanzibar mahali ambapo anaishi mpaka hivi leo.

Mbali na uimbaji Bi.Kidude pia ni mfanyabiashara.Anauza “wanja” na “hina” ambazo anazitengeneza mwenyewe. Pia ni mtaalamu wa dawa za mitishamba lakini zaidi ya yote yeye ni Mwalimu wa “unyago” ambapo anacho chuo chake mwenyewe huku akijivunia rekodi kwamba katika wanafunzi wake wote hakuna ambaye ameshawahi kupewa talaka na mumewe. Pengine hii ndio sababu mwaka 2004 ulipozuka umbea kwamba Bi.Kidude amefariki dunia wakati alipokuwa katika ziara ndefu ya kimuziki Ulaya na Mashariki ya mbali, kila mtu kisiwani Zanzibar alishikwa na butwaa na majonzi! Kwa bahati nzuri habari za “kifo” chake zilikuwa ni uzushi tu.

Leave a Reply