Utata umegubika suala la mtu anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi Padre Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki baada ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Zanzibar kuinyima Polisi kibali cha kumfikisha mahakamani.
Mtu huyo, Omar Mussa Makame wa Zanzibar alitarajiwa kupandishwa kizimbani juzi, lakini ofisi ya DPP ilikataa hiyo hiyo juzi kutoa kibali kwa Polisi kufanya hivyo. Omar aliwahi kugombea ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha Wananchi (CUF) jimbo la Rahaleo mwaka 2010.
Awali Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema jana kuwa wameshindwa kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo kwa vile DPP hakuwapa kibali.
Alipulizwa sababu ambazo zimemfanya DPP asitoe kibali hicho, alisema ni vyema akaulizwa yeye mwenyewe kwani ndiye aliyetoa sababu hizo.
Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim alipofuatwa ofisini kwake jana ilielezwa kuwa yuko kwenye mkutano na mwandishi wa habari hizi akalazimika kumuandikia juu ya suala hilo kupitia kwa Katibu Muhtasi wake.
Alijibu kwa njia ya maandishi majibu yake yakiwa na maneno matatu tu: “Kamuone Kamishna Mussa”.
Alipoandikiwa tena kuwa Kamishna Mussa ndiye aliyesema uulizwe wewe kwani ndiye uliyetoa sababu alijibu kupitia kwa Katibu Muhtasi wake: “Yeye (Kamishna) anazijua sababu kwanini hataki kuzisema? Nendeni kwake mukamuulize”.
Alipoulizwa mara ya pili juu ya majibu hayo ya DPP Ibrahim, Kamishna Mussa alisema kwamba yeye hawezi kujibu mambo ya mtu mwingine.
“Ndio majibu yake ninayo, lakini yeye (DPP) ndiye aliyetoa sababu kwa hiyo ndiyo yeye anayetakiwa kuzisema sio mimi, nadhani hii ndiyo haki, aseme mwenyewe,” alisema Kamishana Mussa.
Mtuhumiwa huyo yuko mikononi mwa Polisi tangu Machi 17 mwaka huu alipokamatwa kuhusiana na mauaji hayo ya Padre Mushi aliyeuawa Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Katika hatua nyengine Mahakama Kuu Zanzibar imeamuru kuletwa mahakamani kwa mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi, jumatatu ijayo ili kuweza kusikiliza shauli lililofunguliwa juzi na mawakili wa upande wa mlalamikiwa la kutofishwa mahakamani kwa mteja wao ndani ya saa 24 baada ya kukamatwa.
Mtuhumiwa huyo Omar Mussa Makame (37)aliyekuwa mgombea uwakilishi wa Jimbo la Rahaleo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) bado anashikiliwa na polisi Zanzibar, anatetewa na Kampuni ya Uwakili ya AJM Solicitors and Advocate.
Juzi mchana wakili wa Kampuni hiyo Abdalah Juma Mohamed aliwakilisha mahakama kuu ya Zanzibar maombi ya Habeas Corpus application chini ya kifungu cha 390 cha Sheria ya Makosa Jinai sura ya 7 ya mwaka 2007 inayomtaka mtu anayemshikila mtu mwingine au chombo chochote bila kumfikisha mahakamani kwa saa 24 aeleze mahamaka sababu za kushikilia mtu bila kumfikisha mahakamani au amwachie huru.
Mawakili hao walimtumia summons Mkurugenzi wa Mkosa ya Jinai Zanzibar (DCI) na jana Naibu wake Kamishina Msaidizi wa Polisi Yusuf Ilembo alifika mbele ya Jaji Isack Mkusa, kusikiliza shauli hilo.
Mawakili wa Kujitegemea upande wa mlalamikiwa waliokwakilishwa na Shabani Juma Shabani pamoja na Shaibu Ibrahim waliiomba mahakani hiyo iamuru kuachiwa kwa mteteja wao .
Hata hivyo jaji Mkusa alisema, kutokana na maombi hayo kuletwa chini ya kiapo vi vema pia Upande wa serikali nao ukapewa muda wa kujiandaa kuweza kujibu hoja hizo chini ya kiapo.
Baada ya kusikilza pande zote mbili Jaji Mkusa chini ya kifungu cha sheria section 8 ya mwaka 2006 inatoa nafasi kwa mtu kupewa dhamana lakini kwa jinsi mahakama itakanyoona inafaa.
Lakini wakati huo huo muhusika naye aletwe mahakamani wakati wa kusikiliza shauri lake ‘application’ kulingana na section 8.
Padre Mushi aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Kanisa la Minara Miwili Zanzibar aliuawa asubuhi ya February 17 mwaka huu kwa kupigwa risasi wakati akijiandaa kuendesha ibada katika kanisa la Mtakatifu Theresia nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Kuuawa kwa risasi kwa Pandri Mushi, kulitanguliwa pia na shambulizi kama nilo kwa Padri Padri Ambrose Mkenda pia wa Kanisa Katokiki Zanzibar mwezi desemba mwaka jana ambaye alijeruhiwa taya ya kulazwa kwa siku kadhaa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wakati huo huo Ofisi ya DCI Zanzibar, imesema bado inasumbiri pia majarada mawili ya kesi ya kumwagiwa tindikali kwa 6 Nov 2012 kwa Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga, pia lile la Padri Ambrose Mkenda ambayo bado yapo kwa DPP ili kuwafikisha mahakamani watu wanaotunumiwa na makosa hayo mbao kwa sasa wako nje kwa dhamana.
Chanzo: Mwananchi