Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

AL-SHABAAB YATISHIA KUSHAMBULIA MIKOA YA KASKAZINI MASHARIKI YA TANZANIA



KUNDI la kigaidi nchini Somalia lenye uhusiano na al Qaeda, la al Shabaab limetishia kufanya mashambulizi Tanga na Kilimanjaro na tayari vyombo vya usalama mkoani Kilimanjaro, vimetoa hadhari katika maeneo ya viwanda vinavyoweza kushambuliwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Absalom Mwakyoma, alithibitisha kuwapo kwa tishio hilo lakini alikataa kuzungumzia zaidi kwa madai ni la kiusalama zaidi.

“Hilo jambo lipo lakini sitalizungumzia, kwani ni mambo ya kiusalama zaidi…wewe nani amekupa taarifa hizo, muulize aliyekwambia akufafanulie,” alisema.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Mtendaji Utawala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC, Jaffary Ali, wamepewa taarifa za kuchukua hadhari juu ya kuwapo kwa tishio la shambulio kiwandani hapo.

Alisema taarifa hizo zimetolewa na Kamanda Mwakyoma baada ya kupata taarifa mbalimbali za kiusalama zilizopatikana juu ya kuwapo kwa tukio hilo.

“Ni kweli tumepata taarifa za kuwapo kwa shambulio la kikundi cha al Shabaab lakini haijataja moja kwa moja kwamba sisi ndio tunashambuliwa ila tumetakiwa kujihadhari na watu, magari na hata pikipiki, tusizozifahamu,” alisema.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Mwakyoma, huenda kikundi hicho kikatekeleza mashambulizi yao kwa kutumia pikipiki, jambo ambalo linasababisha kutilia shaka vyombo vyote vya usafiri vinavyopita kiwandani hapo.

Alisema kutokana na taarifa hizo, tayari kiwanda kimetoa hadhari kwa wafanyakazi wake, viongozi wa vijiji vinavyozunguka kiwanda pamoja na familia za wafanyakazi kuwa makini
dhidi ya watu wasiowafahamu.

“Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda, kwa Tanga kimetajwa kiwanda cha saruji, lakini huku kwetu tumehadharishwa katika maeneo haya ya viwanda, kwani ndiyo lengo lao, tumewataka wafanyakazi wasiwe na hofu, lakini pia tunaendelea na kazi,” alisema.

Alisema menejimenti imeimarisha ulinzi katika eneo la kiwanda, lakini pia imeagiza mbwa maalumu wa kutambua mabomu kutoka Arusha ili kusaidia ukaguzi wa maeneo yote.

Alisema wafanyakazi wa mashambani wamepewa taarifa kuhusu ubebaji miwa, kwani huenda
wakabeba bomu na kuliingiza kiwandani, iwapo kikundi hicho kitatega kupitia mashamba.

"Hawa mbwa tulioagiza watafanya doria maeneo yote ya kiwanda na mashamba kutokana na
hofu kwamba wakitumia mashamba ni rahisi kuyabaini," alisema.

Kwa upande wao, baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TPC, waliojitambulisha kwa jina moja la Mziray na Juma, walisema tishio hilo limeleta hofu, kwani athari za mashambulizi ya kikundi hicho ni makubwa.

Alisema wameshuhudia mara kadhaa kupitia vyombo vya habari, katika nchi za Kenya na Uganda, jinsi ambavyo vimeshambuliwa na kikundi hicho na kusababisha vifo vya mamia ya wananchi wasio na hatia.

"Hili tishio limetulazimu kuhamisha baadhi ya wanafamilia wetu, tumewataka waende mjini
Moshi kuishi na ndugu," alisema.

Akizungumzia taarifa hizo, mkazi wa kijiji cha Langasani wilayani Moshi vijijini, Abdul Sultan, alisema ni vyema Serikali ikaimarisha usalama katika mipaka ili kudhibiti kikundi hicho.

Alisema pamoja na suala la mipaka ya nchi, lakini pia zipo sababu za msingi kwa wananchi kupewa elimu ya utambuzi wa watu wenye nia ovu ili iwasaidie kukabiliana na watu hao.

Kikundi cha al Shabaab kimekuwa kikifanya vitendo vya ugaidi ndani ya Somalia, Uganda na Kenya hata kulazimu majeshi ya Kenya kuingia nchini Somalia kukabiliana nacho.
[ Read More ]

Don’t be sad. Allah knows everything.






I leave and go, but Allah ‘the one with all the kindness is always there

And I ask Him for hope that is never rejected

And I ask Him for safety from a world

I am tested through it, where it’s disasters turn me gray

And I ask Him all the time and in all cases

Because He is the one who makes our hearts feel safe

The way He makes everything around is beyond our imagination

It is mysterious to us, because it is the fate to be

It is Allah who eases things for us, but it is beyond our knowledge

And easing hard tragedy on us

And from generosity and hidden kindness

As well as solutions to hardships we face

I have no one to ask but Allah

He is my only Lord and the only one my heart is full of love for

He is generous, blessing, kind and answers the prayers of His slave

He covers up His slave’s sins and answer who ever ask Him

He is patient, forgiving and always put forgiveness before punishment

He is so merciful that His merciful includes all beings

Oh Lord, forgive me

My sins distanced me from You

My mistakes and sins sicken me more everyday

But You’re the only doctor that can make me feel fine

Oh Allah, keep those who envy away from me and make me feel safe

Disasters do indeed hurt

Bless me with the company of my children and family

Because it is easy for anyone to feel lonely

Give me the strength, when my powers faint

And inspire me to mention and praise You throughout my life

I gain my strength and my hopes from the richness of whorshipping You

                               Allah is always there
[ Read More ]

Sita Wafariki kwa Kula Kasa Micheweni

    WATU sita wamefariki dunia Tumbe wilaya ya Micheweni Pemba na wengine kulazwa hospitali wakiwa hali zao mbaya baada ya kudaiwa kula nyama ya kasa.

Taarifa kutoka kisiwani humo zinaeleza kuwa waliofariki katika mkasa huo wakiwemo watoto ni pamoja na Sara Hamad Bakar (55), Aisha Said Juma (7), Fatma Abdalla Rajab (5), Mariyamu Said Juma (5), Nasria
Khatib Haji (1) na Zuwaifa Omar Khamis (6).


Waliolazwa katika hospitali ya Chake Chake ni pamoja na Said Juma Khatib (45) ambaye ndiye mvuvi wa kasa huyo, Said Juma Khatib (20), Rehema Bakari Simba (25), Mwanakhamis Hamad Mwijab (70), Mkitu Haji Abeid (48) na Zaina Juma Khatib (22) ambaye ametibiwa na kuruhusiwa kutoka.

Kasa huyo alivuliwa kutoka baharini Januari 3 mwaka huu, ambapo baada kuchinjwa huko huko baharini alitengezezwa na kuletwa nyumbani kwa ajili ya kitoweo.

Habari kutoka Pemba zinaeleza kuwa baada ya kumla kasa huyo, iliwachukua saa 3 kuanza kupata athari za nyama yake kwa kuugua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Hemed alithibitisha tukio hilo na kuwataka wananchi waache ukaidi kwa kula nyama ya kasa.

Alisema wananchi wakiendelea na ukaidi kwa maagizo yanayotolewa ndipo madhara yanapojitokeza jambo ambali huathiri jamii.

Hadi jana watu watano maiti zao zilikwisha kabidhiwa kwa na kuzikwa na ndugu na jamaa zao.
[ Read More ]

Mimi bado ni CUF – Hamad Rashid

hamad-rashid

Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohammed
Baada ya chama cha CUF nchini Tanzania kumfukuza uwanachama Mbunge Hamad Rashid , Mbunge huyo aibuka na kusema yeye bado mwanachama halali wa chama hicho. Anaeleza mambo yakiwa mabaya zaidi upande wake ataanzisha chama kipya cha siasa.
Sudi Mnette amezungumza na Mbunge huyo wakati akifanya mkutano wake na waandishi wa habari muda mfupi uliyopita jijini Dar es salaam leo hii.
[ Read More ]

Ni uamuzi wa kihuni asema-Hamad

 nje-hamad



 Mbunge wa Wazi Zanzibar Hamad Rashid Mohamed (katikati),akiwa na wanachama wenzake katika kikao cha Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF)mjini Zanzibar jana, kabla ya kuanza kwa kikao cha kuamua hatma yao ndani ya Chama hicho, ambapo anatuhumiwa yeye na wenzake 13 kukisaliti Chama
HATIMAYE Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake watatu wamefukuzwa uanachama wa CUF kuanzia jana. Hatua hiyo ilichukuliwa na zaidi ya robo tatu ya wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika kikao chake kilichofanyika hapa. Uamuzi huo umekata mzizi wa fitina wa hatma ya Hamad na washirika wake hao kisiasa ndani ya chama hicho, baada ya kuibuka mvutano wa muda mrefu kati yake na uongozi wa juu.
Mvutano huo uliochomoza zaidi baada ya Hamad kutangaza kuwania nafasi ya Katibu Mkuu inayoshikiliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad.
Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa na Hamad ambaye ameiita kuwa ni ya kihuni kwani imekiuka amri ya Mahakama iliyotangaza kusitishwa kwa kikao kilichochukua uamuzi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alithibitisha kuvuliwa uanachama kwa Hamad na kuwataja wengine walioondolewa pia kuwa ni Mjumbe wa Baraza Kuu (Tanga), Doyo Hassan Doyo, Mjumbe wa Baraza Kuu (Pemba), Shoka Khamis Juma, Mjumbe wa Baraza Kuu Unguja, Juma Saanane na Mjumbe wa Baraza Kuu (Mbeya), Yassin Mrotwa.
“Kwa mujibu wa katiba ya chama, wasioridhika na uamuzi huo wanaweza kukata rufaa kwenye mkutano mkuu wa taifa,” alisema.
Naibu Katibu Mkuu CUF Zanzibar, Ismail Jussa akizungumza jana jioni na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Ujerumani (DW), alisema haoni kama hatua hiyo ya kuwafukuza wanachama hao akiwamo Hamad ambaye aliwahi kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kunaweza kuhatarisha mustakabali wa chama hicho.
“Ni kweli Hamad ametoa mchangao mkubwa ndani ya chama. Lakini wakati mwingine unapima faida na hasara sasa hivi Hamad alikuwa anaelekea kuvuruga chama,” alisema Jussa
Hamad: Ni uamuzi wa kihuni
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Hamad alisema anashangazwa na kiongozi wa nchi (Maalim Seif), kushindwa kuheshimu amri ya Mahakama na kuendelea na kikao ambacho ilikuwa imeamuru kisitishwe.
“Kiongozi wa nchi anakaidi uamuzi wa mahakama… uamuzi huu mimi nauita ni uamuzi wa kihuni, nimekwenda kwenye kikao naulizwa maswali ambayo wao wamejipanga na mashahidi wao mimi sijajipanga, sina shahidi nawaambia wanipe maswali ili nipate muda wa kuyajibu na kuandaa mashahidi kama wao hawataki, sasa demokrasia ipo wapi hapo?” alisema Hamad.
Hamad alisema hati ya kusimamishwa kwa kikao hicho ilifika ukumbini hapo saa 6:10 mchana, lakini wajumbe wa kikao hicho walionekana kuipuuza na kuendelea nacho na hati iliyopelekwa makao makuu ya Dar es Salaam saa 2:00 jana ilikatiliwa kupokewa akidai kwamba ni kwa agizo kutoka kwa viongozi wakuu.
Alisema hati ya mahakama inaonyesha kwamba wanatakiwa kwenda mahakamani Februari 14, mwaka huu na kusema kwamba uamuzi wa kuaminika utatolewa huko kwani katika chama hicho wanachama wengine wanaonekana hawana nguvu kama katibu mkuu.
Alisema wanachama wote wa CUF wanapaswa kufurahi kwani hajaumizwa na uamuzi kwa kuwa viongozi wake wamekuwa wakionekana kuhubiri haki sawa huku wakienda tofauti na msimamo wa chama.
“Maalim Seif kila siku anaonekana anahubiri haki sawa kumbe hana lolote, anakandamiza tu watu kwa kuharibu chama na kutoa maamuzi kibabe. Mimi sipo tayari kuburuzwa, wakitaka tuelewane haki wanayoihubiri iwe inatendeka kweli,” alisema Hamad.
Kwa upande wake, Shoka Khamis ambaye alikuwa Mbunge wa Micheweni, Kaskazini Pemba katika Bunge la Tisa, alisema kwa mujibu wa katiba ya CUF hamjui aliyemtuhumu kwani haiwezekani mtu asomewe shtaka bila kujua anayemtuhumu.
“Nimejifundisha mengi sana CUF mazuri na mabaya, lakini leo kwa sababu wamenifukuza ngoja niseme mabaya, CUF sisi ni CCM B kama wanavyosema wenzetu. Chama kina sifa mbaya ya kufukuza watu, lakini anayefukuza wenzake, Seif Sharif Hamad yeye anajiona kama mungu hafanyi makosa,” alisema Shoka.
Alisema hawapo tayari kujiunga na chama chochote cha siasa kama maneno yanavyosambazwa kuwa watahamia Chadema. Alisema watafufua Chama Cha Wananchi (CCW) ambacho kiliungana n Kamahuru na kuipata CUF.
“Tuna mpango wa kuanzisha chama kingine kwani CUF kwa sasa kimeshakuwa chama cha mtu ambaye ni Seif na siyo cha wananchi kama kinavyojulikana katika siasa za nchi hii,” alisema Shoka.
Hamad na hujuma
Desemba 27, mwaka jana Hamad aligoma kuhojiwa na Kamati ya Maadili na Nidhamu, akitoa sababu tano huku akiibua tuhuma nzito za kunasa waraka wa mawasiliano uliotumwa kwa barua pepe na Maalim Seif kwenda kwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ukionyesha mpango wa kumshughulikia.
Sababu ya pili, alisema baadhi ya walioteuliwa katika kamati hiyo ya Nidhamu na Maadili walikwisha mtuhumu hadharani na kumtia hatiani hivyo, kikao hicho kisingeweza kumtendea haki.
Alitaja sababu nyingine ya kukataa kuhojiwa kuwa ni kutoelezwa tuhuma zake hasa vifungu vya Katiba alivyodaiwa kuvikiuka.
Pia alitaka apewe hadidu za rejea za kikao kilichounda Kamati ya Nidhamu na Maadili kwa sababu haipo kikatiba, hakuna chombo kama hicho. Aligoma pia kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa tayari alibaini njama za kumshughulikia zilizosukwa na Maalim Seif na Lipumba.
Hamad Rashid alijikuta kwenye mgogoro huo baada ya kutangaza dhamira yake hiyo ya kugombea nafasi ya katibu mkuu mwaka 2014.
Kuanzia hapo akajikuta ameingia kwenye mgogoro na chama hicho kiasi cha kunusurika kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akigawa misaada katika matawi ya chama hicho, Kata ya Manzese.

Chanzo ni Mwananchi
[ Read More ]

HAMAD RASHID

pix  
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limepitisha uamuzi wa kuwafukuza uanachama Hamad Rashid Mohamed, Doyo Hassan Doyo, Shoka Khamis Juma, na Juma Said Saani. Pia limempa karipio kali Yasin Mrotwa.
[ Read More ]

WAUWAJI WA STEPHEN LAWRENCE WABAINIKA!


Baada ya miaka 18 ya upelelezi na kuendesha kesi kuhusu mauwaji ya kijana mweusi mjini London, Stephen Lawrence, wanaume wawili wamepatikana na hatia.


Gary Dobson na David Norris
Gary Dobson na David Norris

Gary Dobson na David Norris wamepatikana na hatia na jopo la mahakama baada ya kesi hio kutegemea ushahidi wa kitaalamu.
Wataalamu wa uchunguzi wa damu na alama kama hizo waligundua alama ya damu kwenye koti la Dobson ambalo bila shaka halingepatikana bila kumkaribia marehemu.

Wakati akiondolewa mahakamani, aliliambia jopo kua wamemhukumu mtu asiye na hatia. Hukumu itasomwa siku ya jumatano.


Stephen Lawrence
Stephen Lawrence

Wazazi wa marehemu Stephen, Doreen na Neville, waliangua kiliyo jopo lilipotangaza kua watuhumiwa wamepatikana na hatia. Duwayne Brooks, rafiki mkubwa wa Stephen Lawrence aliyekua naye waliposhambuliwa, alituma ujumbe kupitia mtandao wa Tweeter akisema, hatimaye, sheria imetendeka'
Mamake Dobson, Bi.Gary Dobson, aliyeiambia mahakama kua mwanawe alikua nyumbani wakati wa mauwaji, aliangua kilio mahakamani kufuatia tangazo la watuhumiwa kupatikana na hatia.

Upelelezi wa kwanza uliofanywa na polisi ulishindwa na kupelekea Polisi ya mji wa London kutuhumiwa kama Idara inayoendesha ubaguzi wa rangi.

Stephen Lawrence alikua mwenye umri wa miaka 18 alipouawa kwa kisu akiwa karibu na kituo cha basi cha Eltham, London ya kusini mnamo mwezi April mwaka 1993. Polisi walitambua watu watatu ambao baadaye walitajwa katika ripoti ya uchunguzi kama washukiwa wakuu.

Hadi wakati huo kulikuepo mfululizo wa mapungufu ya polisi kwa kushindwa kukusanya ushahidi wa kutosha mbara mbili, wa kwanza uliowasilishwa na wazazi wake Stephen Lawrence, Doreen na Neville Lawrence.

Lakini katika kuichunguza kesi hio kwa mda wa miaka minne, wataalamu wengine wa kupeleleza ushahidi waliweza kugundua ushahidi ulioweza kuwaunganisha washukiwa na mauwaji - ushahidi ambao ulia mikononi mwa polisi kwa kipindi kirefu.

Ushahidi huo wa alama za damu, nyuzi za nguo na unywele wa marehemu - vilipatikana kwenye nguo za washukiwa zilizotekwa tangu mwaka 1993.

Wataalamu wa upelelezi wa ushahidi walifanikiwa kugundua ushahidi huo kwa kutumia mitambo ya kisasa ambayo wakati ule havikuwepo.

Dobson, mwenye umri wa miaka 36, na Norris,akiwa na umri wa miaka 35, walikanusha madai ya kuua. Walidai kua damu hio ilichanganyika na nguo zao kutokana na kuchanganywa na ushahidi kupitia kipindi cha miaka mingi.

Wapelelezi walitumia mda kuchunguza jinsi ushahidi huo ulivyozungushwa na jinsi ulivyohifadhiwa kuondoa shaka ya uwezekano wa kuchanganywa kama walivyodai watuhumiwa.

Gary Dobson alikamatwa na kufungwa jela mnamo mwaka 2010 kwa kushiriki biashara ya kuuza mihadarati. Yeye ni miongoni mwa kundi dogo la wanaume waliohusishwa na uhalifu mmoja baada ya Mahakama ya rufaa kuzima ombi lake la rufani mnamo mwaka 1996.

Katika mahojiano marefu na BBC, Mamake Stephen Lawrence, Doreen alisema: "siwezi kuwasamehe vijana waliomuua mwanangu Stephen. Wao hawadhani kama wametenda uovu wa aina yoyote.

Hukumu inatazamiwa sku ya jumatano.habari ya BBC

[ Read More ]

SIMU YA MCHINA YAMLIPUKIA NA KUMUUNGUZA MWILI




Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (kulia) akimjulia hali mfanyabiashara wa mafuta katika Kijiji cha Luilo Ludewa, Joseph Haule ambaye amelipuliwa na mafuta baada ya simu yake ya kichina kulipuka,majeruhi huyo anatibiwa katika Hospital ya Wilaya ya Ludewa, mkoani Iringa.
Filikunjombe na baadhi ya wananchi wakimjulia hali Joseph Haule
Joseph Haule akiwa amelazwa Hospitali baada ya kujeruhiwa vibaya.

[ Read More ]

POLISI ZANZIBAR WAZIMA JARIBIO KUBWA LA UJAMBAZI





Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, limefanikiwa kuzima jaribio kubwa la ujambazi lilokuwa lifanyike mara baada ya kuchukuliwa kwa mishahara ya watumishi wa hoteli moja ya Kitalii.

Afisa Habari wa Jeshi hilo Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa jaribio hilo limezimwa na Polisi jana Alhamisi Desemba 29, 2011 majira ya saa 7.00 mchana baada ya makachero wa Jeshi la Polisi kupata taarifa mapema na kuweka mtego uliowanasa majambazi watatu kati ya sita.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa majambazi wapatao sita wakiwa na silaha aina ya SMG walijipanga kumteka mhasibu wa Hoteli ya Kitalii ya Blue Bay iliopo Kiwengwa huko Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kamanda Aziz amesema majambazi huo walipanga kufanyika uporaji huo mara baada ya kuchukuliwa kwa mishahara hiyo ya watumishi wa Hoteli ya Blue Bay na tukio hilo lingefanyika njiani wakati mhasibu huyo akitokea katika Tawi la Benki ya Barclays lililopo eneo la Kinazini Mjini Zanzibar na Hoteli ya Blue Bay ya Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema majambazi hayo yalifika eneo la tukio wengine wakiwa kwenye gari dogo na wengine wakiwa kwenye pikipiki za kukodi mbili za kukodi vyombo ambavyo viliegeshwa pembeni mwa barabara inayoelekea Bububu wakimsubiri Muhasibu wa Hoteli ya Blue Bay atoke Benki ili wampore fedha hizo ambazo zilikuwa za kigeni.

Hata hivyo Kamanda Aziz amesema kuwa katika tukio hilo ulifanyika ukamataji salama ambao haukuhusisha matumizi ya silaha na hivyo kunusuru maisha ya majambazi kwa upande mmoja lakini pia na kwa Polisi.

Kamanda Aziz amesema Polisi wamefanikiwa kuzima tukio hilo baada ya kuwa na taarifa za kutosha kutoka kwa wasiri wake ambao ni wananchi.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi, kwa kupitia falsafa ya Polisi Jamii, walipatie taarifa sahihi zitakazowezesha kukamatwa watuhumiwa waliotoroka nakuwataka watu wote wanaokwenda Benki kwa dhamira ya kuweka au kuchukuwa fedha nyingi wawe wasiri na kutoa taarifa Polisi ili wapatiwe usindikizaji salama wa fedha zao.
[ Read More ]


[ Read More ]