Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Mama ajinyonga kwa wivu

-
Rehema Mwinyi.

MKAZI wa Kijiji cha Ukata katika kata ya Ukata wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, Bi. Rehema Ndunguru (40) amejinyonga na kufa kwa kinachosadikiwa ni kutokana na mgogoro wa mapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda amesema tukio hili lilitokea Juni 8, mwaka huu saa 3 asubuhi kijijini humo.

Alisema, Bi. Ndunguru alikutwa akiwa amejinyonga chumbani kwakwe kwa kutumia kanga na chanzo kimetokana na wivu wa kimapenzi ambapo imedaiwa mara nyingi alikuwa akimtuhumu mumewe kuwa si mwaminifu katika ndoa yao.

Alifafanua kuwa wakati mama huyo anajinyonga mume wake hakuwepo na kwamba watoto wake waliokuwa wakicheza nje walipoingia ndani walimwona mama yao akiwa ananing'inia chumbani na kutoa taarifa kwa majirani waliotoa taarifa Polisi.

Bw. Kamuhanda ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Leave a Reply