Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Shahidi aeleza maiti ya albino alivyookotwa

-
Rehema Mwinyi.

KESI inayowakabili washitakiwa wa mauaji ya albino mkoani Shinyanga iliendelea kusikilizwa jana ambapo shahidi wa kwanza alianza kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji Gadi Mjemas wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Akitoa ushahidi huo huku akiongozwa na wakili wa Serikali Bi. Veritas Mlay shahidi huyo Bw. Mayenga Matongo ambaye alikuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Harawa alidai kuwa Desemba 4 mwaka juzi akiwa ofisini kwake alipokea taarifa kutoka kwa Yusuph Ramadhani kuwa kuna maiti imeonekana imetupwa katika mto Kidamlida.

Bw. Matongo alidai baada ya kupokea taarifa hizo aliandika barua kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isanga Bw.Sayi Gamanya kumtaka aende kuangalia sehemu ya tukio ili kuthibitisha tukio hilo.

Aidha Shahidi aliongezea kuwa Bw. Gamanya hakutii agizo hilo ndipo shahidi alikwenda na baadhi ya watu katika mto wa kidamlida na kuanza kuusaka mwili ambapo saa 12:00 jioni Mei 4 mwaka jana walifanikiwa kuuona ukiwa kwenye kisima cha kunyweshea mifugo.

Bw.Matongo aliendelea kudai kuwa alitoa taarifa polisi wa Wilaya ya Bariadi Aprili 5 saa 7 mchana polisi walifika eneo hilo na zoezi la kuutoa mwili huo lilianza ambapo ilikutwa imekatwa kichwa na miguu yote miwili na kuhifadhiwa kwenye mfuko wa ambao ulikuwa umeanza kuoza.

Matongo alidai kuwa Diwani wa kata hiyo Bw. Juma Mapilipili kwa kushirikiana na wananchi wengine waliweza kuutambua mwili huo kuwa ni wa marehemu Lyaku Willy ambapo polisi walianza upelelezi wao ambapo iligundulika Mboje Mawe na Masahi Magumba waliokuwa wakiishi kijijini hapo walikuwa hawaonekani.


Alidai kuwa Desemba 6 mwaka jana alipata taarifa kuwa watuhumiwa hao walikuwa wamejificha katika milima ya kijiji cha Harawa na aliwachukua wanamgambo wawili wa vijiji vya Nkwindabuye na Harawa ili kumsaidia kazi ya kuwatafuta watuhumiwa hao.

Alidai tarehe hiyo hiyo majira ya jioni wanamgambo ho waliweza kumkamata Mboje kwenye milima ya kijiji cha Harawa ambapo
inadaiwa aliwataja watu wengine alioshirikiana nao katika mauaji hayo kuwa ni Sayi Mafizi,Chenyenye Maganyale,Sayi Gamanya,Gumbo Nzige na Masihi Magumba.


Kesi hiyo iko Mbele ya Jaji wamahakama Kuu ya Tanzania Bw. Gadi
Mjema ambapo mashahidi wanaendelea kutoa ushahidi wao. Hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa mwezi ujao.

Leave a Reply