SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeunda tume ya watu 8 kuchunguza chanzo cha ajali ya Mv. Fatih ambayo ilisababisha vifo vya watu 6 pamoja na hasara ya mali.
Akitangaza kuundwa kwa tume hiyo, Waziri wa Nchi, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Bw. Machano Othman Said alisema tume hiyo imepewa kazi ya kujua chanzo cha ajali ya Mv Fatih
Bw. Machano alisema tume hiyo imepewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha kazi yake na kuwasilisha ripoti kwa wizara husika ambapo Mwenyekiti wa tume hiyo ni Jaji Omar Makungu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar akisaidiwa na nahodha mkongwe ambaye, Meneja Mkuu wa Shirika la Meli la Zanzibar Alhaji
Masoud Sururu.
Wajumbe wengine katika tume hiyo ni Bw. Abdalla Kombo, Bw. Mohamed Mahmoud Juma, Bw. Nahodha Hatib
Katundula kutoka katika kikosi cha jeshi la majini la KMKM, Meneja wa Ufundi wa Shirika la Bandari Zanzibar, Bw. Abdi Maalim.
Meli ya Mv Fatih ilipata ajali wakati ikikaribia eneo la Bandari ya Malindi mjini Zanzibar ambapo watu 34 walifanikiwa kutoka katika chombo hicho na wengine kuokolewa baada ya kuzama baharini.
Categories: