Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Washabiki 12 Wa Michael Jackson Wajiua Kufuatia Kifo Chake

-
Rehema Mwinyi.


Msichana mmoja wa nchini Tunisia amejiua kwa kumeza vidonge kutokana na huzuni ya kifo cha Michael Jackson huku ikikadiriwa kuwa jumla ya washabiki 12 wa Michael Jackson kutoka sehemu mbali mbali duniani wameishajiua tangia kutangazwa kwa kifo chake. Msichana huyo wa mji wa El Manar uliopo kaskazini mwa Tunia alijiua kwa kunywa vidonge vingi sana baada ya kugubikwa na huzuni kubwa tangia habari za kifo cha Michael Jackson zilipotangazwa.

Taarifa zilizema kwamba msichana huyo alitumia siku nzima akiwa amejifungia chumbani kwake akiangalia video za Michael Jackson kabla ya kuamua kunywa vidonge hivyo na kufariki.

Michael Jackson alifanya shoo yake ya kwanza kabisa barani Afrika nchini Tunisia mwaka 1996 iliyohudhuriwa na washabiki wake 65,000.

Jumla ya watu 12 washabiki wakereketwa wa Michael Jackson kutoka sehemu mbali mbali duniani inasemekana wamejiua baada ya kutangazwa habari za kifo cha Michael Jackson.

Gary Taylor, rais na mmiliki wa tovuti ya MJJcommunity.com, iliyoanzishwa miaka kumi iliyopita alisema kwamba anavyofahamu hadi sasa washabiki 12 wa Michael Jackson ambao walihuzishwa sana na kifo chake wamejiua.

"Ninavyofahamu ni kwamba watu 12 wamejiua sehemu mbali mbali duniani, mmoja wapo ni raia wa Uingereza" alisema Taylor.

"Hali imekuwa mbaya, watu wanachukua uamuzi wa haraka ambao Michael asingetaka washabiki wake wauchukue, angewataka waendelee kuishi", alisema Taylor.

Jesse Jackson, rafiki wa karibu wa Michael ametoa video kwenye YouTube akiwataka washabiki wa Michael wasijidhuru.

Wakati huo huo taarifa za kutoka nchini Urusi zilisema kwamba mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Pável Talaláyev alijaribu kujiua muda mfupi baada ya kutangazwa kwa kifo chake na baada ya jitihada kubwa za madaktari kunusuru maisha yake alipozinduka alianza kuwalaumu madaktari kwa kumuokoa na kusema "Hili ni pigo kubwa sana kwangu, sitaki kuishi tena sijui kwanini wameniokoa nataka nikawe pamoja na Michael".

Leave a Reply