Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Ajali zaua watatu Jijini

-
Rehema Mwinyi.

Watu wa watatu wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa vibaya katika ajali za barabarani zilizotokea katika maeneo tofauti Jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumzia kuhusiana na tukio la kwanza, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye amesema lilitokea saa 9:30 usiku wa kuamkia jana katika barabara ya Haile Selasi, maeneo ya Oysterbay na kulihusisha gari aina saloon lenye namba za usajili T 555 AJV.

Amewataja waliofariki kuwa ni dereva wa gari hilo na mkazi wa Upanga, Jalvad Gama , 32 na abiria mmoja mkazi wa Masaki aliyetambuliwa kwa jina la Sailen Gilan, 50. Amesema katika ajali hiyo mtu mmoja aitwaye Gurminber Jandu , 30 alijeruhiwa.

Kamanda Kalunguyeye amesema ajali hiyo ilitokea baada ya dereva aliyekuwa akitokea Masaki kwenda barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kushindwa kulimudu gari na kugonga mti.

Amesema miili ya watu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Aghakhan.

Amesema majeruhi huyo ambaye ni mkazi wa Masaki na fundi magari, anaendelea na matibabu katika hospitali ya Aghakhan.

Katika tukio la pili, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile amesema mwenda kwa miguu mmoja amefariki dunia baada ya kugongwa na gari lisilofahamika.

Amesema ajali hiyo ilitokea jana saa 12:15 asubuhi katika eneo la Tazara wakati mwenda kwa mguu huyo ambaye ni mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30-35, alipokuwa akivuka barabara ya Nyerere.

Amesema gari wala dereva aliyemgonga hakufahamika na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Leave a Reply